Friday, June 8, 2012

MADUME YA ARUSHA YALAZIMISHA KUWAINGILIA KINYUME CHA MAUMBILE WATOTO WA MITAANI ARUSHA


HII NI MOJA YA PICHA YA WATOTO WA MITAANI WAKIWA WAMELALA NDANI YA MAENEO MBALIMBALI YA NCHI YA TANZANIA



STORY NA UPAKO WA HABARI

WATOTO wanaoishi mazingira magumu na hatarishi ndani ya Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani Mjini Arusha wameomba Serikali na Mashirika mbalimbali kuwasaidia kwa kuwa wapo baadhi ya watu wazima ambao wanataka kuwaingilia kinyume cha maumbile kwa kisingizio kuwa ni watoto wasio na waangalizi

Hayo yamebainishwa na watoto hao wakati wakiongea na “UPAKO WA HABARI”katika eneo la pembezoni mwa Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani ndani ya Jiji la Arusha mapema jana.

Wakizungumzia Tatizo hilo watoto hao walisema kuwa wanalazimika kuogopa sana hasa nyakati za usiku kwa kuwa wapo baadhi ya watu wazima ambao wanawataka kinyume cha maumbile na kudai kuwa watawapa fedha ambazo ni kati ya 1000-  2000 mara baada ya kufanya tendo hilo

Walisema kuwa  hali hiyo inawatisha sana na kuwafanya wengine kukosa amani hasa nyakati za usiku kwa kuwa wanapokataa kufanya matendo hayo hulazimika kupigwa na hata mara nyingine watu hao wazima kuwaambia watoto wenzao kuongeza kipigo

“huwa tunaogopa sana hata kujilaza katika mitaro kwa kuwa hawa watu ambao ni kama baba zetu na wengine kama babu zetu wanapokuja kutuomba kufanya nao tendo hilo sisi tunakataa kwa kuhofia kuumia na hata kupata Ukimwi sasa tunaomba Ushirikiano uwepo baina yetu sisi na Polisi watakapokuja tu washikiliwe kwa kuwa hata sisi tunahaki ya kuishi”walisema watoto hao


Wakati huohuo watoto hao waliiomba wamiliki wa vyoo hasa katika maeneo ya stendi hiyo kuwasaidia kuwapa huduma za vyoo bure kwa kuwa wanalazimika kutumia mifuko midogo na kisha kujisaidia haja kubwa hali ambayo ni hatari hata kwa afya zao

Watoto hao waliongeza kuwa hali hiyo mbali na kuwa ni hatari kwa afya zao pia inachafua hata hali ya usafi wa jiji kwa kuwa wanalazimika kutupa vinyesi hivyo kwenye barabara kuu za jiji la Arusha huku Mji wa Arusha ukiwa unapiga kelele za usafi

“tunapowaomba wamiliki wa vyoo watusaidie tuweze kujisaidia hata haja ndogo wanatukatalia badala  yake wanatuambia kuwa tuwe na 200 sasa kama hakuna mtu aliyetupa siku hiyo tunatumia mifuko na kisha tunatupa vinyesi hivyo  bila hata mpangilio maalumu”walisema watoto hao

MWISHO

No comments:

Post a Comment