Saturday, June 30, 2012

WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WAKUSUDIA KUNUNUA KIWANDA CHA CHAI KATUMBA

WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WAKUSUDIA KUNUNUA KIWANDA CHA CHAI KATUMBA

 

habari na francis godwin 

Kiwanda kinachokusudiwa kununuliwa na wakulima wadogo wa chai Rungwe
Wakulima wakichuma chai yao
Timu ya wanahabari kutoka mkoa wa Iringa na Dar
WAKATA wakulima wadogo wa chai wilayani Mufindi na Njombe wakiendelea kulia na unyanyasaji wanaoupata kutoka kwa makampuni makubwa ya chai kwa kununua chai yao chini ya kiwango ,chama cha wakulima wadogo wa chai wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanatarajia kununua kiwanda cha wakulima Tea Compani (Katumba ) ili waweze kukimiliki kama njia ya kuepukana na manyanyaso ya makampuni dhidi ya wakulima wa zao hilo imefahamika.

Wakulima hao wadogo wa chai Rungwe wamefikia hatu hiyo kama njia ya kuepukana na manyanyaso ambayo wameendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na kuuza chai yao kwa bei ya chini zaidi .


Akizungumza na timu ya wanahabari mwenyekiti wa chama hicho cha wakulima wadogo wa chai Rungwe Johnson Mwakasege alisema kuwa pamoja na changamoto mbali mbali ambazo wakulima wa chai wamekuwa wakizipata ila kwa upande wa wakulima wa chai Rungwe wameendelea kunufaika zaidi na kilimo cha chai kupitia msaada mkubwa wanaoupata kutoka taasisi ya utafiti wa chai Tanzania (TRIT) kwa hisani ya jumuiya ya Ulaya (EU) hivyo wamepanga kuepuka manyanyaso hayo na hivyo kukusudia kununua kiwanda cha chai Katumba ili waweze kumiliki wenyewe.

Alisema kuwa kwa sasa wakulima hao wa chai wadogo wanamiliki kiwanda hicho kwa hisa alisimilia 30 na asilimia 70 inamilikiwa namwekezaji huku mipango yao kwa mwakani kuweza kumiliki hisa zote 100 katika kiwanda hicho.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa kiwanda hicho cha katumba wanakusudia kununua kwa shilingi bilioni 2.6 na tayari mazungumzo yameanza na ikiwezekana mwakani 2013 wakulima hao wataanza kuendesha kiwanda hicho.

Kwani alisema kuwa lengo la wakulima wa chai Rungwe ni kuweza kuwawezesha wakulima kuwa na sauti kubwa katika kiwanda hicho na kuweza kuongeza malipo ya chai kutoka shilingi 206 ambazo wanalipwa sasa na kufikia bei nzuri zaidi itatayomwamasisha mkulima kuweza kupanua mashamba zaidi ya chai .

Hata hivyo alisema kuwa chama hicho cha wakulima wadogo wa chai Rungwe kwa sasa kina mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kutoka kiasi cha shilingi milioni 10 ambazo wakulima hao walikuwa nazo mwaka 1998 walipo anza umoja huo .

Mwakasege alisema kuwa mbali ya kukusudia kununua kiwanda hicho bado wakulima hao wadogo wameweza kujenga ofisi yao ya kisasa kwa kiasi cha shilingi milioni 500 kama njia ya kujiimarisha zaidi .

Aidha alisema kuwa chama hicho cha wakulima wa chai Rungwe kimetenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI wilayani humo ili kupunguza vifo vya vijana vinavyotokana na ugonjwa wa UKIMWI na kupelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa na kuwaacha wazee wakiendelea kubeba mzigo mkubwa wa kuhudumia mashamba ya chai .

MWISHO

No comments:

Post a Comment