Monday, June 11, 2012

milion 200 za wanufaisha wajasiamali

KAMPUNI ya Tanzania browaries Limited(TBL) imetoa ruzuku ya vitendea kazi vyenye gharama ya shilingi milioni mia mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Tanzania nzima huku kanda ya kaskazini ikikabidhiwa vitendeakazi vyenye gharama ya shilingi milioni 50 lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuzisaidia jamii mbali mbali zinazowazunguka.

Akikabidhi vitendea kaz i hivyo kwa wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini katika tamasha lililofanyika mjini hapa meneja wa bia ya safari larger bw Oscar Shelukindo alisema kuwa kampuni hiyo imejiwekea mpango wa kuhakikisha kuwa wanawasidia wajasiriamali Tanzania nzima ili waweze kujikwamua katika hali ngumu ya kiumskini.

Alisema kuwa vifaa hivyo walivyovitoa kwa wafanyabiashara hao ni vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kutumika katika biashara zao mbali mbali wanazoziendesha kwa kuwa wako watu wana malengo na maono mazuri ya baishara lakini wanashindwa kufikia malengo kwa ajili ya kukosa vitendea kazi.

“sisi tumeona tuwe na mpango endelevu wa kuwasaidia hawa wafanyabiashara vitendea kazi mfano yuko huyu mfugaji wa kuku tumempatia mashine,mwingine friza ambapo kila mmoja anategemea biashara anayofanya alimaradi tu wamekidhi vigezo vyetu lazima tumapatie vitendea kazi “alisema Shelukindo

Aliongeza kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ambapo ametaja kanda ambazo zinahusika na kupatiwa vitendea kazi kuwa ni pamoja na kanda ya kusini ,mwanza, dares saalam pamoja na kanda ya kaskazini ambapo aliwataka wafanyabiashara kujitokeza mwaka huu kujaza fomu kwa kuwa endapo watakidhi vigezo vinavyohitajika nao wataweza kunufaika na vitendea kazi vya kuendeshea biashara zao.

Awali mgeni rasmi katika tamasha hilo afisa biashara manispaa ya arusha bw Niarira Elivelema alisema kuwa swala hilo lililofanywa na Safari Larger ni mfano wa kuigwa na taasisi nyinginezo kwa kuwa wameonyesha ushirikiano wao na jamii inayowazunguka .

Aliongeza kuwa endapo wafanyabiashara wadogo watapewa kipaumbele kama walivyofanya tbl ni wazi kuwa hata taifa nalo litaweza kuongeza kipato kutokana na ushuru ambao utakuwa unalipwa kutoka kwa wafanyabiashara hao.

mwisho

No comments:

Post a Comment