Tuesday, June 5, 2012

WAIMBAJI WATAKIWA KUACHA KUENDEKEZA ZAIDI MASLAHI



WAIMBAJI wa nyimbo za injili wametakiwa kufanya kazi hiyo ya uimbaji kama njia ya kutangaza injili hasa katika maeneo ya vijijini na kuacha kufanya kazi ya injili kwa maslahi kwa kuwa wapo wachungaji  na makanisa yao ambayo yanashindwa kufikiwan na huduma ya  uimjbaji kwa kuwa hayana fedha za kuwalipa waimbaji

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Mchungaji Anthony Albert “Joka Kuu”katika kania la EAGT Moria wakati akizungumza na waumini wiki iliyopita mara baada ya kuweka wakfu  cd ya waimbaji wa kanisa hilo inayojulikana kwa jina la Bado Kitambo

Mchungaji Anthony alisema kuwa wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili ambao kwa sasa wameendekeza zaidi maslahi ya uimbaji na kusahau kuwa uimbaji ni wito na hali hiyo inachangia kudidimiza hata maisha ya wakristo ambao hawana uwezo

Alifafanua kuwa kwa sasa makanisa ambayo yanaonekana kuwa na uwezo wa kuwaita waimbaji hao  ni makanisa yale ambayo yanaweza kuwalipa lakini kwa makanisa hasa ya vijijini huwa hayana nafasoi ya kuita na kuwatiumia waimbaji hao maarufu

Aliongeza kuwa hali hiyo si makusudio ya Mungu na kwa hali hiyo waimbaji wanatakiwa kuwa makini na kuhakikisha kuwa wanarudi katika fasheni za biblia na wala sio fasheni za maslahi kama walivyo baadhi ya waimbaji kwa sasa

“unakuta kanisa au huduma inamujita muimbaji lakini kwa kuwa kanisa lile halina uwezo wa kumuita Muimbaji  sasa kama hawa waimbaji wameitwa kwa ajili ya watu wenye fedha je hawa maskini wanakwenda wapi ni lazima waimbaji wafike mahali wajue na kutambua kuwa wao wapo kwa ajili ya kueneza injili na wala sio kwa ajili ya kuangalia maslahi”alisema Mchungaji Anthony.

Awali alisema kuwa nao wanakwaya wa makanisa mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika maisha ya kiroho na kuachana na tabia ya kuwa Moto Baridi ndani ya makanisa na badala yake wanatakiwa kuimba kwa mujibu wa biblia inavyosema na kudai

Aliongeza kuwa nao  wanakwaya wa sasa baadhi yao huwa wanaaimba kwa mazoea hali ambayo inawafanya wengi kila mara kujikuta wakiwa wanaanguka katika dhambi kubwa ikiwemo dhambi ya uzinzi  ambayo inawatesa walio wengi sana.

”nawasihi sana ninyi wanakwaya hakikisheni kuwa kamwe hamrudi nyuma hakikisheni kuwa hamshindani  kimavazi kwa kuwa mnaposhindana kwa mavazi hamfikii hata malengo yenu ya kuifikisha injili panapotakiwa”alisema Mchungaji Anthony


MWISHO

No comments:

Post a Comment