Monday, June 18, 2012

WAONESHENI WAHALIFU UPENDO NA PIA WAPENI ELIMU

Na Queen Lema,ARUSHA

IMEELEZWA kuwa machafuko ndani ya jamii nyingi yanazidi kuongezeka kwa
kuwa asilimia kubwa ya wanajamii waliowengi wanawatenga wahalifu
mbalimbali badala ya kuwapa elimu ambayo itawafanya waweze kuacha
uhalifu wao

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Steve Robert Kutoka Tanga wakati
alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha kwa Muorombo Kata ya
Terrat Mkoani Arusha mapema jana

Bw Robert alisema kuwa kwa sasa hakuna elimu yoyote ambayo inatolewa
kwa watu ambao wanahasi jamii hali ambayo inawafanya hata baadhi yao
kutengwa huku uhalifu ukiwa unakithiri sana

Alifafanua kuwa endapo kama jamii ingekuwa na Muongozo imara hasa
katika eneo hilo la Kwa Muorombo basi hata idadi ya uhalifu nayo
ingepungua sana kwa kuwa kila mara wahalifu wa matukio mbalimbali
wangeweza kupatiwa mafunzo pamoja na madhara ya uhalifu

Alisema kuwa mtu ambaye ni muhalifu hapaswi kutengwa na jamii yake na
badala yake jamii inatakiwa kuonesha na kuimarisha zaidi upendo ili
waweze kufikia katika hatua za kuacha uhalifu ambao ndio chanzo
kikubwa sana cha umaskini

“leo hii unakuta eti mtu ni muhalifu lakini badala ya kupewa elimu
mbalimbali ya kumsaidia jinsi ya kuepukana na tabia hiyo anatengwa na
jamii na wakati nafasi mbalimbali zinatakiwa kutumikan ikiwemo nafasi
ya mashirika na Taasisi za Dini”aliongeza bw Robert

Pia aliongeza kuwa wananchi wanapswa kujua mbinu pekee ya kuweza
kukinzana na uhalifu wa aina mbalimbali ndani ya jamii husika ni
kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kuanzia ngazi za familia kwa kuwa nazo
familia nyingi hazina utaratibu wa kuwaelezea watoto wao madhara ya
kuwa waharibifu na wavunjifu wa amani

Awali alitataja madhara ya kukithiri kwa uhalifu hasa wizi mdogo mdogo
kuwa ni pamoja na kuwepo kwa majanga makubwa sana ya umaskini ndani ya
jamii wakati taifa lina buni mbinu mbalimbali za kupambana na
Umaskini.

MWISHO

No comments:

Post a Comment