Monday, December 31, 2012

WAOMBA KUPANDISHIWA HADHI ZAHANATI ALIYOZINDUA MAMA NYERERE MWAKA 1964


WAOMBA KUPANDISHIWA HADHI ZAHANATI ALIYOZINDUA MAMA NYERERE MWAKA 1964

Na Queen Lema,MERU

SERIKALI imeombwa kupandisha hadhi zahanati ya kata ya Majengo wilayani Meru mkoani Arusha ambapo zahanati hiyo ilizinduliwa rasmi na kupewa misaada na Mama Maria Nyerere mwaka 1964 huku malengo ya Mama huyo yakiwa ni kubadilika kutoka zahanati na kuja kituo cha afya kwa haraka sana jambo ambalo mpaka sasa halijafanyiwa kazi.

Hayo yamebainishwa na Paulo Mayeke ambaye ni katibu kata ya Majengo,wakati akiongea na Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha waliotembelea Kata hiyo na kuzindua Kata mpya ya chama cha mapinduzi mapema jana.

Aidha bw Mayeke alisema kuwa Zahanati hiyo ya Majengo ilizunduliwa Rasmi na Mama Nyerere huku lengo halisi la Mama huyo likiwa ni zahanati hiyo isidumu kama zahanati na badala yake iwe kwenye mfumo wa kituo cha afya ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi hata wa vijiji vya Jirani kwa kuwa Kata hiyo ipo Karibu sana na Machimbo ya madini ya Tanzanite

Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama Serikali ya sasa itakumbuka na kurejea kauli na ahadi  ya Mama Maria Nyerere basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana kuraisisha shuguli za afya ndani ya Kata hiyo ambayo imedumu na zahanati badala ya kituo cha afya kwa muda mrefu sana huku jamii nayo ikiendelea kukabiliwa na Magonjwa mbalimbali.

Alisema kuwa endapo kama itakuwa katika mfumo wa Zahanati basi itachangia sana kuokoa maisha ya watu kwani itakuwa na wataalamu wengi wa afya tofauti na sasa ambapo kutokana na hadhi yake inawahudumu wachache sana wa Afya hali ambayo inachangia sana wananchi kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma hizo.
“jamani hii zahanati ya kata ya Majengo ilizinduliwa na kupewa mikakati mbalimbali na Mama Nyerere kwa mwaka 1964 lakini moja ya msisitizo wake mkubwa ilikuwa ni kuwa katika hadhi ya kituo cha afya lakini toka siku ile ameondoka Kijijini hapa hakuna kilichoendelea hivyo basi tunaomba Serikali itusaidie kwani Wananchi wetu wanapata shida kubwa sana ya matibabu na hivyo kama watafanya hivyo wataweza okoa maisha ya watu wengi zaidi”aliongeza Bw Mayeke

Awali mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Bw Onesmo Nangole alisema kuwa watendaji wa chama hicho kuanzia ngazi ya Vitongoji mpaka mkoa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatatua na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi sanjari na kutafutia ufumbuzi jambo ambalo litaweza kuwafanya wananchi kuwa katika kundi moja la chama hicho

Bw Nangole aliongeza kuwa tabia ya Viongozi kukaa kimya na kusinzia huku wakijiita ni viongozi haipaswi kuvumikila kwani tabia hiyo ndiyo inayochochea Kero kubwa sana kwa wananchi na hata mara nyingine kusababisha ahadi mbalimbali zishindwe kutekelezwa huku wananchi nao wakielekeza lawama kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)

“Nawasihi sana Viongozi kuanzia ngazi ya chini kuamka kuanzia sasa acheni kuwapa wapinzani nguvu kwa kero za wananchi mbona mnauwezo wa kuweza kufanya mabadiliko na changamoto hata ahadi mbalimbali mkazifuatilia,kwa kuwa sasa hivi changamoto yoyote ile kwenye jamii ndio nguvu ya wapinzani sasa hakikisheni kuwa hawa wapinzani wanakosa nguvu kabisa”aliongeza Bw Nangole

MWISHO

No comments:

Post a Comment