Friday, December 14, 2012

MKUU WA WILAYA AKERWA NA WANAOLALAMIKA OVYO JUU YA UTENDAJI WA SHUGULIZA MAZINGIRA ARUSHA

MKUU WA WILAYA AKERWA NA WANAOLALAMIKA OVYO JUU YA UTENDAJI WA SHUGULIZA MAZINGIRA ARUSHA

MKUU wa Wilaya ya Arusha bw John Mwongela amewataka wananchi wa jiji
la Arusha kuachana na tabia ya kulalamika ovyo juu ya mamlaka ya Jiji
na badala yake wahakikishe kuwa kabla ya kulalamika wanatoa mawazo
ambayo yanachangia maendeleo ya usafi wa Jiji

Bw Mongela aliyasema hayo leo katika mdahalo baina  ya  viongozi
mbalimbali wa Serikali na wadau wa mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya
Kiserikali mkoani arusha(ANGONET)ambapo mdahalo huo ulihusiana na
masuala ya mazingira kwa mkoa wa Arusha.

Bw Mongela alisema kuwa dhana kubwa sana ndani ya Mkoa wa Arusha kwa
sasa  ni ulalalamishi na manunguniko juu ya Jiji na utendaji kazi wake
jambo ambalo linafanya hata baadhi ya watu kushindwa kuonesha ufanisi
zaidi katika masuala mbalimbali yakiwemo mazingira.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watu ambao wanalalamika juu ya
masuala mbalimbali ya Jiji wanasahu kuwa ulalalamishi wao unatakiwa
kwenda sanjari na mawazo ambayo yatachochea vyanzo hivyo vya
ulalamishi kufa ingawaje kwa sasa hadi watendaji wa Serikali nao
wanalalamika juu ya Jiji.

‘kwa sasa kila mahali ambapo utakwenda utasikia watu wanalamika nah ii
sio kwa watu binafsi bali ni hadi kwa watendaji wa Serikali nao
wanalalamika sana sasa kama wote tutaishia kulalamika je nani atakuwa
ni mtendaji wa hayo malalamiko, mimi nadhani kuwa huu ni muda sasa wa
kufanya mabadiliko kwa kuhakikisha kuwa tunatoa mbinu za kukabiliana
na changamoto na wala sio kulalamikalamika ovyo’aliongeza bw Mongela.

Awali Afisa mali asili wa mazingira kwa jiji la Arusha Bw Njwaba
Mwajibe alisema kuwa mbali na dhana hiyo ya kulalamika juu ya utendaji
kazi wa jiji hususani kwenye suala zima la mazingira lakini bado
wananchi wana matatizo ya kutoweka mazingira kwenye hali ya usafi.

Bw Mwajibe alisema kuwa hali hiyo inasababisha sana baadhi ya mitaa
kuonekana michafu ambapo wanaotupa uchafu husingizia jiji chafu huku
magonjwa ya mlipuko nayo yakiwa yanawasonga wananchi .

‘unakuta mtu anatoka na uchafu kwake anautupa nje ya nyumba yake
halafu anadai kuwa jiji ni chafu sasa sisi jamani tutaingia ndani ya
majumba ya watu na kusafisha inabidi wananchi wa Arusha wabadilike na
wahakikishe kuwa wanakuwa wasafi kuanzia ndani ya majumba
yao’aliongeza Bw Mwajibe.

Alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa Jiji limejipanga kuhakikisha kuwa
waharibifu wa mazingira wanafikishwa katika vyombo vya dola ikiwemo
mahakama ya jiji ambayo itaanza kazi hivi karibuni hali ambayo itaweza
kuufanya mji wa Arusha kuwa safi zaidi kama yalivyo  majiji mengine.

No comments:

Post a Comment