Monday, December 3, 2012

BINTI ANAYEKISIWA KUANGUKA NA UNGO ANGANI KWA NJIA ZA KISHIRIKINA AWEKWA CHINI YA ULINZI WA KANISA


 NA MWANDISHI WETU,MERU

BINTI mmoja ambaye hakuweza kutambulika jina mara moja  mwenye umri wa
kati ya miaka 18 hadi 20 yuko chini ya ulinzi wa kanisa la huduma ya
injili ya Neema lililopo Nshupu wilayani Arumeru mara baada ya
kudondokea hapo kwa mazingira ya kishirikina.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumfanyia maombi ya kumfungua
binti huyo,mchungaji wa kanisa hilo Elly Mafie alisema kuwa binti uyo
alidondokea kanisani hapo novemba 21 majira ya saa tisa alasiri akiwa
katika hali ya kutatanisha.

Alisema kuwa binti huyo ambaye alisadikikia kuwa ni msukule na
hajafahamika alikotokea alidondoka hapo akiwa hajitambui na hawezi
kujieleza kwa lolote hali ambayo iliwafanya wakazi wa eneo hilo kutaka
kumwua kwa kumchoma kwa moto lakini mchungaji huyo alimwokoa na
kumpeleka sehemu ya usalama zaidi ili kuweza kufanyiwa uchunguzi.

“kwa kweli naweza kusema kuwa huu ni mpango wa mungu wa kumwezesha
binti huyu aweze kupatiwa uponyaji kupitia maombi kwa kuwa alikuwa
hajitambui kabisa na hawezi hata kuongea hii inaonyesha ni jinsi gani
alikuwa amefungwa na vifungo vya shetani  lakini naamini atafunguka na
kujieleza kadri tutakavyokuwa tiunamfanyia maombi “alisema Mafie
.
Aliongeza kuwa kupitia hali aliyokuwa nayo binti huyo  waumini wa
kanisa hilo walilazimika kufanya maombi ya kumfungua binti huyo ambapo
baada ya maombi hayo aliweza kurudiwa na fahamu kidogo kidogo huku
akidai kuwa ametokea Moshi na ametumwa na mkuu wake.

Alifafanua kuwa awali binti huyo alipodondokea hapo alikuwa katika
hali ya kusitisha kwa kuwa alikuwa katika hali ambayo sio ya
kibinadamu pamoja na mambo ya ajabu aliyokuwa akiyatenda .

“mungu amemeleta huyu binti kwa kusudi lake ili roho yake ipate
uponnyaji hivyo tunaamini atafunguliwa na ninawaomba kila mtu
aendeleaa kumwombea na hatimaye ndugu zake wajitokeze ili waweze
kumchukua kwa kuwa huenda nao wanateseka kumtafuta au pengine wanajua
alishakufaga siku nynigi”

Hata hivyo ameelitaka kanisa kuwa macho kwa kuwa hizi ni nyakati za
mwisho kwa kuwa watayaweza yote kwa yeye atiwaye nguvu.
mwisho

No comments:

Post a Comment