Monday, December 10, 2012

WASIOTUMIA ARDHI MERU KUNYANGANYWA NA KUPEWA WATU WENYE UHITAJI-MKUU WA WILAYA



WASIOTUMIA ARDHI MERU KUNYANGANYWA NA KUPEWA WATU WENYE UHITAJI-MKUU WA WILAYA

Na Queen Lema, Meru

WILAYA   ya Meru inatarajia kuboresha  mipango mbalimbali  ya matumizi bora ya ardhi ambapo pia itawanyanganya mashamba wamiliki wa mashamba makubwa ambao hawayatumii na badala yake mashamba hayo yatatumika kwa matumizi mbalimbali ya ardhi

Kauli hiyo imetolewa Wilayani humo na mkuu wa wilaya hiyo bw Munasa Nyirembe wakati kiongea na wananchi wa wilaya hiyo ndani ya maazimisho ya Miaka hamsini na moja ya wilaya hiyo mapema jana

Bw Munasa alisema kuwa mikakati ambayo ipo kw sasa ndani ya wilaya hiyo ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajua vema matumizi ya ardhi bora ingawaje wapo baadhi ya wananchi na wawekezaji ambao hawatumii mashamba na badala yake kuyaacha hivyo hivyo

Alisema kuwa mpngo huo wa kuchukua ardhi ambazo hazitumiki kwa muda mrefu utaweza kusaidia sana kuraisisha maendeleo ya wilaya hiyo kwani bado wapo watu wengi sana ambao wanakabiliw na uhaba wa ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali huku matumizi hayo ya ardhi bora yakiwa ni moja ya vichocheo vya uchumi wa Nchi

“pamoja na kuwa tuna mikakati ya aina mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tuna kuwa na matumizi bora ya ardhi lakini pia hii itasadia sana kwa kuhaikisha wale ambao wana nunua ardhi kwa muda mrefu bila kutumia wataweza kutumia tena kwa njia ambayo itaweza kukuza na kuimarisha uchumi waWilaya kwa kuwa wengine wananunua ardhi na kuacha huku wenzao wakikosa ardhi  kwa ajili ya matumizi mbalimbali’aliongeza Bw Munasa.

Pia alisema kuwa mkakati mwingine ambao utaweza kuboresha wilaya hiyo hasa katika masuala ya uchumi ni pamoja na suala zima la upimaji wa ardhi ambao utaenda sanjari na suala zima la utoaji wa hati miliki tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa hakuna suala la hati miliki za viwanja

“kwa kipindi kirefu sana wananchi wameteseka hata kwa kunyimwa mikopo ndani ya taasisi mbalimbali za fedha lakini kama watapata haki miliki basi wataweza kuzitumia kwa ajili ya mikopo hivyo tunaamini kabisa hili suala litaweza kuongeza ufanisi wa kiuchumi ndani ya vijiji vyetu na hata wilaya yetu kwa ujumla’alisem Munasa

Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na kuchukua viwanja ambavyo havitumiki pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa kwenye sekta ya Kilimo  kwa kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la eneo linalolimwa hasa kwenye mazao ya chakula kutoka hekta 80,000hadi kufikia hekta 121,387 sawa na asilimia 51.73

Bw Munasa alisema kuwa ongezeko hilo limesababisha changamoto kama vile kilimo kisichozingatia hifadhi ya ardhi na maji,bei kubwa za pembejeo na tatizo la soko la kuaminika kutokana na bei ndogo zinazotolewa.

Alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo Wilaya kwa sasa imeamua kutumia mbinu mbalimbali kama vile kutumia teknolojia za kisasa,kuanzisha na kuimarisha ushirika wa vyama vya kuweka na kukopa kwa ajili ya kupata mitaji na kutafuta masoko

MWISHO

No comments:

Post a Comment