Monday, December 10, 2012

UKOSEFU WA MIUNDO MBINU IMARA KWA AJILI YA WALEMAVU NDANI YA MAKANISA NA MISIKITI CHANZO CHA WALEMAVU KUSHINDWA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA



UKOSEFU WA MIUNDO MBINU IMARA KWA AJILI YA WALEMAVU  NDANI YA MAKANISA NA MISIKITI CHANZO CHA WALEMAVU KUSHINDWA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA

Na Queen Lema,Aruha

IMEELEZWA kuwa kutokana na baadhi ya taasisi mbalimbali za dini hapa nchini kushindwa kujenga majengo ambayo yanakidhi haja za walemavu kumesababisha walemavu wa viungo kusindwa kupata haki zao za msingi za kuabudu huku hali hiyo ikisababisha madhara kwa jamii

Changamoto hiyo imetolewa mjini hapa katika kanisa la St James na walemavu wa viungo mbalimbali ambao walihudhuria ibada maalumu kwa ajili yao iliyofanyika kanisani hapo mapema jana

Walemavu hao wa Viungo walisema kuwa inasikitisha kuona kuwa asilima kubwa ya makanisa pamoja na misikiti ikiwa imejengwa bila kukumbuka aina ya ulemavu wao huku wakiwa wanasisitzwa kwenda kuabudu ingawaje hakun mazingira rafiki ambayo yanaweza kuwafariji

Walisema kuwa majengo mengi ya ibada ni magorofa na baadhi ya walemavu hawana viungo kama vile miguu ambapo hali hiyo inawafanya washindwe kupanda kwenye ngazi kutoana na aina ya ulemavu wao jambo ambalo linawafanya wakose haki zao za msingi  ya kuabudu

‘tunapenda sana kuja makanisani na hata misikitini lakini tnapofikiria miundo mbinu ambayo siyo rafiki kwetu kweli tunakata tamaa ingawaje sehemu mojawapo ya kutufariji ingekuwa ni kwenye nyumba hizo za ibada sasa tunawaomba wakuu wote wa taasisi hizi wawe na tabia ya kutufikiria kwa kuhakikisha kuwa na sisi tunapewa nafasi ya kuabudu  kama ilivyo sheria ndani ya Katiba ya Nchi’waliongeza walemavu hao wa viungo.

Awali Mchungaji Kiongozi  wa kanisa hilo bw Andrew Kajembe alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa kila Taasisi ya dini inawakumbuka walemavu ingawaje  kwa sasa asilima kubwa ya taasisi za dini zimewasahau walemavu kwa hofu mbalimbali hali ambayo inawafanya waone kama wametengwa na jamii zao huku matendo ya unyanyasaji dhidi yao nayo yakiwa yanaongezeka siku hadi siku

Bw Kajembe alisema kuwa hata miundombinu ya baadhi ya makanisa bado si rafiki sana kwa walemavu hivyo basi wakuu wa makanisa wanatakiwa kuhkikish wakati wanafikiria kujenga pia waweze kuwafikiria walemavu  ambao wamesahulika ingawaje ndani ya makanisa na taasisi za dini ndipo wanapoweza kupata faraja ya maisha ikiwemo dhana ya uwajibikaji kwa shuguli za kijamii zaidi.

“Sisi kama wakuu wa makanisa na misikiti bila kujali itikadi zetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawasaidia hawa walemavu kwa kuimarisha majengo yetu na yawe rafiki kwa maisha yao na pia hata ndani ya ibada zetu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunawatengea hawa walemavu siku maalumu kwaajili yao na sadaka zote ziweze kuelekezwa kwao kwani  kwa kufanya hivyo bila kujali dini zao itasadia sana kuongeza ufanisi kwao na hata maisha yao kuweza kuboreka zaidi”aliongeza bw kajembe

Wakati huo huo alisema kuwa siku hiyo ya walemavu pia ilenda sambamba na siku ya kuwafariji wagonjwa ambapo waumini wa kanisa hilo walitembelea na kuwafariji wagonjwa na majeruhi wa hospitali ya Mt Meru pamoja na watoto waliozaliwa katika hospitali ya Levolosi.

No comments:

Post a Comment