Monday, December 17, 2012

KATA ZA MBUGUNI NA MARORONI WILAYANI MERU ZIMEATHIRIWA VIBAYA NA MABADILIKO TABIA NCHI

KATA ZA MBUGUNI NA MARORONI WILAYANI MERU ZIMEATHIRIWA VIBAYA NA MABADILIKO TABIA NCHI

Na Queen Lema,MERU

IMEELEZWA kuwa Kata za Mbuguni na Maroroni katika wilaya ya Meru mkoani hapa imeathirika vibaya sana kutoka na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kufanya shuguli mbalimbali za kilimo na mifugo kukwama kwa muda mrefu sana

Hayo yalielezwa na afisa mifugo wa wilaya hiyo Bw Mohamed Hassan wakati akiongea katika mdahalo wa mazingira hususani tabia nchi uliondaliwa na mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa (ANGONET)mapema jana

Bw Mohamed alisema kuwa kata hizo ambazo zipo kusini mwa wilaya hiyo ni moja ya kata ambazo zimeonekana kuwa na madhara makubwa sana ya tabia Nchi kutokana na sababu mbalimbali hali ambayo hata kwa upande mwingine imesababisha Ukame

Alisema kuwa kitu kikubwa ambacho kimesababisha maeneo hayo ya kusini mwa wilaya hiyo kukumbwa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na mabonde pamoja na Mafuruko ambayo yanahamisha hata rutuba ya udongo tofauti na maeneo mengine ndani ya Wilaya ya Meru

Aliongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikizaa matunda mabaya sana ya ukame ambapo baadhi ya mazao yameshindwa kustawi huku baadhi ya mazao kama vile mihogo na Mtama yakistawi kwa shida hivyo kuruhusu umaskini mkubwa sana kwa kata hizo ambazo ni tegemezi ndani ya mkoa wa Arusha.

“kwa kweli hapa Meru hii hali imetuathiri sana kwa kuwa hapo awali haya maeneo yalikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha lakini sasa hawawezi kuzalisha kwa wakati hivyo ukame na umaskini ndio umekithiri sana ingawaje sisi kama sisi tuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tunaokoa haya maeneo ambayo yameathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi”alisema

Awali mratibu wa mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa Bw Peter Bayo alisema kuwa kuna ulazima mkubwa sana wa kuhakikisha kwanza jamii inakuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi pamoja na na uharibifu wa mazingira yanachangia sana kudidimiza uchumi wa nchi na
atajamii


Bw Bayo alisema kuwa endapo kama jamii itakuwa na uelewawa mambo hayo itakuwa ni raisi sana kuweza kuchukua tahadhari mapema sana hasa wananchi wa Vijijini tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya wananchi hawana elimu ya vyanzo vya mabadiliko hayo hali ambayo inachangia sana madhara ndani ya jamii.

Mbali na hayo aliwataka nao watandeji wa Serikali kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kuwa na midahalo ambayo itawahusisha wananchi na hapo wataweza kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mabadiliko hayo tofauti na pale ambapo wananchi wanapopata fursa pindi wanapokutana na asasi binafsi

MWISHO

No comments:

Post a Comment