Monday, December 3, 2012

Serikali yatakiwa kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi .

waziri wa fedha hapa nchini william mgimwa





Serikali yatakiwa kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi .

Happy Lazaro, Arusha.

SERIKALI imetakiwa kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi kwa nchi za nje huku ikilinganishwa kuwa Afrika ina fursa nyingi  za kutosha ambazo zinatuwezesha kufikia malengo mbalimbali bila ya kuomba omba misaada.

Aidha endapo ukusanyaji kodi inayotokana na VAT itaboreshwa na kulipwa kwa wakati basdi itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupatikana kwa pato kubwa la Taifa ambalo litawezesha nchi kujiendesha yenyewe bila kuwa tegemezi.

Hayo yalisemwa  jana na Waziri wa fedha , William Mgimwa alipokuwa akifungua mkutano wa  wa mamlaka ya mapto katika nchi za Afrika (VADA)  pamoja na wadau walipa kodi inayotokana na VAT kutoka nchi za Afrika uliolenga kujadili  mbinu mbalimbali za kuboresha ukusanyaji kodi .

Alisema kuwa, imefika wakati sasa kwa Tanzania kuondokana na tabia ya kuomba misaada bila sababu wakati tuna fursa nyingi ambazo zikiboreshwa zitawezesha kuongezeka  kwa mapato ya nchi ,hivyo kuwezesha kuongezeka kwa idadi kubwa ya miradi mbalimbali.

Alisema kuwa, ili kuwezesha kufikia malengo hayo walipa kodi wa vat hawana budi kulipa kodi zao kwa wakati bila kukwepa kama sheria ya VAT inavyoeleza huku  ikiwa ni pamoja na kuimarisha uzalishaji , unaolenga kuondoa utegemezi huo .

Alisema kuwa, ili kuboresha ukusanyaji wa kodi kuweza kuongezeka mwaka hadi mwaka na hatimye kufikia malengo waliyojiwekea wanaandaa mikakati tofauti ambayo itaweza kuwasaidia ubadilishaji wa ukusanyaji kodi ili kukusanya kodi ya kutosha.

‘Ili tuweze kufikia malengo yetu na kuondokana na tabia ya kuwa tengemezi kwa kuomba misaada katika nchi zingine ni lazima kodi aina ya VAT iboreshwe ili kuziba mapungufu yaliyopo ili kuwawezesha wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi waweze kulipa na kwa njia hiyo tutaweza kufikia malengo yetu’alisema Mgimwa.

Mgimwa alifafanua zaidi kuwa, lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kubadilishana uzoefu wa jinsi ambavyo wenzetu wanavyokusanya kodi katika nchi zao , na hatimaye kuweza kujiwekea mikakati jinsi ya kuboresha ukusanyaji kodi inayotokana na VAT ili kuongeza pato la nchi na hatimaye malengo yaliyowekwa yaweze kufikiwa.

Aliwataka wafanyabiashara wanaolipa kodi inayotokana na VAT kulipa kwa wakati na kwa hiari ili kuiwezesha nchi kuwa na pato la kutosha na hatimaye fedha zinazotokana na VAT kuweza kusaidia kuboresha miradi mbalimbali na hatimaye kufikia malengo yaliyowekwa.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment