Na Queen Lema,MERU
IMEELEZWA kuwa baadhi ya wananchi hasa wa Vijijini
wanaharibu Mazingira na uoto wa Asili wa Vijiji kutokana na hali ngumu ya
maisha huku wengine wakiwa wanafanya hivyo kutokana na ukosefu wa elimu
mbalimbali hasa elimu ya Mazingira bora hali ambayo inachangia kwa kiwango
kikubwa sana Vijjiji vingi kukabiliwa na Ukame
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoanekoli wilayani
Meru Mkoani hapa Bw Christphoer Palangyo wakati akiongea na “upako wa habari”mapema jana
kuhusiana na hali ya uharibifu wa mazingira ambayo inafanyika ndani ya eneo hilo
Bw Palangyo alisema kuwa hali ngumu ndio chanzo pekee
ambacho kinasababisha baadhi ya wananchi kuharibu mazingira hasa katika eneo hilo la Nkoanekoli hali ambayo kama haitachukuliwa
tahadhari basi itasababisha Ukame wa hali ya Juu sana
Alifafanua kuwa asilimia kubwa ya wananchi hasa wa eneo hilo
la Nkoanekoli wanajishugulisha na shuguli za uchimbaji wa udongo ili waweze
kujikimu na hali ngumu za maisha ya kila siku huku wengine wakiwa wanafanya
hivyo bila ya kujua na kutambua kuwa hali hiyo ni mbaya sana hasa kwa utunzaji
wa Mazingira.
“Elimu ya utunzaji wa mazingira ni muhimu sana hasa kwa maeneo ya vijijini
kwa kuwa baadhi ya watu wanaharibu vyanzo
mbalimbali na malzingira kutokana na hali ngumu ya maisha na pia wengine
hawajui madhara ambayo yanaweza kutokea lakini kama watu wangekuwa wanapewa
elimu ya kutosha basi wasingeweza kuendelea
kuharibu mazingira ambayo ni chanzo kilimo kwanza ambacho nacho kwa sasa
kimedorora sana hasa katika maeneo ya Vijijini”aliongeza Bw Palangyo.
Akiongelea hali ya uharibifu wa mazingira hasa katika maeneo
ya Kijiji ckha Nkoanekoli alisema kuwa kwa sasa wananchi wengi wanachimba
Udongo ili waweze kujikwamua na hali ya Maisha huku hali hiyo ikisababisha kwa
kiwango kikubwa sana
Mmonyoko wa udongo ndani ya Kijiji hicho.
Hataivyo alisema kuwa
kutokana na hali hiyo Uongozi wa kijiji hicho umelazimika kuingilia kati suala
hilo ambapo mpaka sasa uharibifu ni mkubwa sana hasa katika maeneo ambayo yapo
kwenye vyanzo vya maji(CHEMCHEM) huku hali hiyo pia ikichangia kwa kiwango
kikubwa sana baadhi ya vyanzo hivyo kukauka na kubaki vikiwa na hali ya ukame
sana.
“hawa wananchi wa kijiji hiki ambao wanachimba Udongo kwa
sasa wamevamia hadi katika vyanzo vya maji na kuchimba bila kujua kuwa kvyanzo
hivyo ni muhimu sana hata kwan kata nyingine sasa kwa hali kama hii imetulazimu
kuanza kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa nguvu sanjari na kutunga sheria
kali hasa kwa hawa watu ambao ni wachimba udongo kwani kama hali itaendelea
kama hivi baada ya miaka mitano hapa Meru patakuwa ni jangwa kabisa”aliongeza
bw Palangyo
Alimalizia kwa kusema kuwa ni Vema kama Serikali pamoja na
asasi binafsi zikahakikisha kuwa zinajiwekeza zaidi vijijini ambapo ndipo
kwenye uitaji mkubwa sana wa utunzaji wa mazingira na Endapo kama hawataweza
kufanya hivyo basi baadhi ya wananchi kila mara wataharibu mazingira huku
wakijua kuwa wapo sahihi na wanachokifanya kwenye uharibifu huo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment