Kikundi cha vijana cha KIPENET kikimba nyimbo za kuishukuru UN kwa kuwaonyesha Mwanga wa Maisha na Maendele baada ya kupata elimu ya ujasiriamali
Na Queen Lema,Arusha
WAJASIAMALI 4000 WAPEWA ELIMU YA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO
VIDOGO PAMOJA NA VIWANDA VYA KATI
Kampuni inayojihusha na Utengenezaji wa shuguli za Biashara
Tanzania (TBCC)imefanikiwa kutoa elimu kwa wajasimali zaidi ya 4000 kutoka
maeneo mbalimbali Nchini ambapo baadhi yao kwa sasa wanamiliki Viwanda Vidogo
Vidogo pamoja na Viwanda vya Kati huku wakiwa
ni sehemu ya kuchangia Pato la Taifa.
Akiongea na “Majira”jana Jijini hapa Mkurugenzi mtendaji wa
Kampuni hiyo Bw Mchau Elibariki alisema kuwa Wajasiriamali hao wamepata elimu
hiyo kuanzia mwaka 2009 ambapo baadhi yao
kwa sasa wanamiliki Viwanda Vidogo Vidogo
Bw Elibariki alisema kuwa
Kampuni yake imeamua kufanya hivyo kutokana na Nchi kuwa na
Wafanyabiashara wengi ambapo bila kujua
kuwa wao ni wachuuzi hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana hata baadhi ya wadau
wengine wakiwemo wafanyakazi kutopata ajira
Aliongeza kuwa kupitia wajasiamali hao 4000 ambao wameweza
kupata elimu hiyo wengi wao wamekuwa na faida kwa Nchi ya Tanzania kwani wameweza kuongeza
hata idadi ya watu ambao wameajiriwa tofauti na pale ambapo Nchi inakuwa na
wachuuzi wengi kuliko wafanyabiashara
Alifafanua kuwa pamoja na kufanikiwa kuwapa elimu na mbinu
mbalimbali kwa wanajamii bado Kampuni
hiyo ina dhamiria kuendelea kuwapa wananchi fursa za kumiliki Viwanda Vidogo
Vidogo pamoja na Viwanda vya Kati ambapo
hapo napo patakuwa na manufaa makubwa sana kwani hata pato la Taifa nalo
litaweza kuongezeka sana huku Maitaji muhimu ndani ya jamii nayo yakiweza kutatulika
kwa Uraisi kutokana na kipato ambacho kinapatikana.
“Tumedhamiria kuwepo
na Viwanda vya kutosha kila mahali kwani tunao huo uwezo wa kutengeneza bidhaa
zetu na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi kwa kusubiria zaidi bidhaa za nje na
pia kupitia hata viwanda hivyo vidogo vidogo na vya kata pia Tunatarajia hawa
wafanyabiashara wawe na Mtaji ambao haupungui kiasi cha Shilingi Bilioni
Moja”aliongeza Bw Elibariki
Pia alisema kuwa ili kuweza kuwa na wafanyabiashara ambao
watamiliki Viwanda Vidogo na Viwanda vya kati wamedhamiria kwa kipindi cha
miaka Mitano Mitano mfululuzo watakuwa na wafanyabiashara 25 ambao wataweza
kumiliki Viwanda hivyo huku wakiwa na Mtaji wa kiasi cha shilingi Bilioni Moja
kwa kila Mmoja ambapo nao hawa wataweza kuendesha viwanda vyao ambavyo vitakuwa
ni viwanda venye manufaa kwa jamii.
“tukishafanikiwa kuwapa hawa watu wenye Mitaji ya kiasi cha
Shilingi Bilioni moja itakuwa ni raisi sana kwetu kuweza hata kulipa Kodi za
Nchi kwa uraisi tofauti na pale kila mtu anapokuwa na biashara yake ndogo ndogo
ya Uchuuzi na kwa hali hiyo tutaweza kusogeza Nchi kutoka sehemu moja ya
ulipaji wa kodi hadi sehemu Nyingine”aliongeza Bw Elibariki
Bw Elibariki alimnalizia kwa kusema kuwa kwa sasa ni vema
kama kila Mtanzania akafikiria jinsi ya kupata elimu ya ujasiamali ili aweze
kujikomboa dhidi ya Umaskini kwani kupitia masomo ya Ujasiamali yana uwezo wa
kuwafanya walio wengi zaidi kuinuka na kuachana na ktabia ya kuwa Tegemezi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment