picha ya kwanza ni jengo la kanisa la st joseph mfanyakazi mara baada ya baadhi ya waumini wake kupigwa na mabomu
baadhi ya majerui katika tukio hilo
majeruhi wengine tena katika tukio hilo
BALOZI WA VATIKAN ALIPUKIWA NA BOMU,MMOJA AFA WENGINE ZAIDI YA THELATHINI WAJERULIWA VIBAYA KANISANI.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu wasiofahamika wametupa bomu katika kanisa la Roman Katoliki la Mt Joseph mfanyakazi liliopo Olasiti Mjini hapa na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia huku wengine thelathini wakiwa majerui
Bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa na a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika
Akidhibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda
wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo
lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe wa kanisa
hilo jipya
Sabas alisema kuwa wakati balozi huyo anakata utepe
huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo liliweza kuwajerui watu
huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja
"huyu balozi alikuwa
hapa Arusha toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa
kutosha juu yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu
hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo
jipya"alisema Sabasi
Pia aliongeza kuwa mpaka sasa polisi
inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini uchunguzi
unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini pia msaada
wa majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo.
wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa wananchi wa jiji la Arusha
hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano
alisema
kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata
matibabu ingawaje bado kuna ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa
Arusha (Mt Meru)
"kazi ya uchunguzi tunatakiwa kuachia vyombo
vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia
tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa
majerui wameumia vibaya sana"alifafanua Magesa
Wakati huohuo
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya
uharibifu wa makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na
Dar es Saalam lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa
sana ya watu wafe.
Lema alisema kuwa lazima mambo kama hayo
yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu kwenye makanisa
hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna hatari kama
hiyo.
Aliyataka makanisa kuachana na tabia ya kuwa karibu na
wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa wanajitegemea kwa michango yao
wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi kabisa kwenye makanisa.
Hataivyo Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za mount Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu,
Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent
Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew,
Anna Edward, .
Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim.
Wakati huo huo jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.
MWISHO
Monday, May 6, 2013
BALOZI WA VATIKAN ALIPUKIWA NA BOMU,MMOJA AFA WENGINE ZAIDI YA THELATHINI WAJERULIWA VIBAYA KANISANI. Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu wasiofahamika wametupa bomu katika kanisa la Roman Katoliki la Mt Joseph mfanyakazi liliopo Olasiti Mjini hapa na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia huku wengine thelathini wakiwa majerui Bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa na a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe wa kanisa hilo jipya Sabas alisema kuwa wakati balozi huyo anakata utepe huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo liliweza kuwajerui watu huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja "huyu balozi alikuwa hapa Arusha toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa kutosha juu yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo jipya"alisema Sabasi Pia aliongeza kuwa mpaka sasa polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini uchunguzi unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini pia msaada wa majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo. wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa wananchi wa jiji la Arusha hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata matibabu ingawaje bado kuna ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru) "kazi ya uchunguzi tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana"alifafanua Magesa Wakati huohuo Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya uharibifu wa makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na Dar es Saalam lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa sana ya watu wafe. Lema alisema kuwa lazima mambo kama hayo yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu kwenye makanisa hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna hatari kama hiyo. Aliyataka makanisa kuachana na tabia ya kuwa karibu na wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa wanajitegemea kwa michango yao wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi kabisa kwenye makanisa. Hataivyo Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za mount Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, . Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim. Wakati huo huo jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao. MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment