Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Thursday, May 29, 2014

SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA WATOTO

 NA JAMES STANLEY ARUSHA
SERIKALI  imeombwa kuwapatia Bima ya Afya watoto
wanolelewa katika kituo cha kulelea watoto  yatima
cha Samartan Villege,kilichoko Moshono,Mkoa ni Aru
sha.
   Mratibu wa kituo hicho,   Father Josephat Mumany,
akizungumza hivi karibuni wakati wakutoa taarifa fupi
yakituo hicho bkwa viongozi   na wanachama wa kiku
ndu cha uamsho cha Oldadai,waliotembelea kituo hich
o kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali,Alisema   bima
hizo zitwapunguzia adha watoto hao wanapougua.
   Alisema kutokana na watoto hao kutokuwa na Bima
ya Afya,hali hiyo imekuwa ikiupa shida kubwa viongozi
wa kituo hicho,pale unapopataka kuwapeleka  watoto
hao hospitalini.

  Father Mmanyi,alisema hiyo ni changamoto    kubwa
kwao,kutokana na kituo kukabiliwa na  uhabawafedha,
hali amabayo pia huwafanya watotowanaougua kukaa
na maradhi yao kwa muda mrefu pasipo kupata  matib
abu.
  Katika hatua nyingine  Mmanyi alisema watoto wanao
lelewa katika kituo hicho wanapelekwa na serikali baada
ya kuokotwa mitaani,kutokana na kutupwa na    wazazi
wao baada ya kujifungua.
  ''Watoto hawa wanaokotwa katika mazingira  magumu 
wengine wanavunjwa miguu na wazazi wao,    wengine
wanakutwa wametoboleatobolewa na wazazi wao kabla
ya kuwatupa,Inasikitisha sana unapoona mazingira amba
yo watoto hawa walikotoka.''Alisema
   Pamoja na serikali,aliitaka jamii na mashitika mbalimbali
ya kitaifa na kimataifa,kukisaidia kituo hicho kwa hali  na
mali,ili kiweze kumudu malezi ya watoto hao.Hivi sasa.ali
sema wana miradi waliyopewa na wahisani inayowasaidia
katika mambo madogomadogo.Nayo ni pamoja na bwawa
la samaki,shamba la mahindi,pamoja na migomba.
  Mweka Hazina wa kikundi cha Uamsho,kilichowatembele
a watoto hao,Be Marry Mayagila,Alisema wanaguswa  na
amahitaji ya watoto hao na kwamba kwa kuwa wao ni w
anawake wenye moyo wa huruma,ndiyo maana wameme
amua kuwatembea na kuwapatia misaada ya vyakula.

   Alitoa wito kwa wanawake,na vikundi mbalimbali kuwa
hurumia watoto hao kwa kuwapa misaada      mbalimbali
kwani hawawajui wazzi wao,ili nao wajione swa na wato
to wengine

Tuesday, May 27, 2014

HOSPITALI YA MT MERU ARUSHA YAENDELEA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO

HOSPITALI ya Mkoa  wa Arusha, Mount Meru, inakabiliwa na upungufu wa
shuka 300 na blanketi 200, kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa kila
siku.

Akizungumzia upungufu huo jana hospitalini hapo, wakati akipokea
msaada wa shuka nyeupe 100 na blanketi 30 toka kwa Kanisa la Calvary
Temple la Kilombero Jijini Arusha,ambalo linaadhimisha miaka 75 tangu
lianzishwe, Mganga Mfawidi wa Hospitali hiyo, Dk. Josiah Mlay, alisema
upungufu ni mkubwa wa vitu hivyo ukizingatia wanakwenda kipindi cha
baridi kali.

Alisema kuwa shuka na blanketi walizonazo kwa sasa nyingi zimechakaa
kutokana na kemikali wanazotumia kufulia wakati zinapochafuka wodini,
hivyo wanahitaji shuka na blanketi zingine haraka kabla ya msimu wa
baridi haujaanza.

"Kwa nyie kutuletea hivi vitu tunashukuru sana na mtabarikiwa, kwani
bado tuna upungufu wa itu hivi mkubwa na tunaomba wadau wengine
wajitokeze kutusaidia kabla ya msimu wa baridi haujaanza,"alisema.

Dk. Mlay alisema kwa sasa hospitali hiyo inachangamoto kubwa ya
ongezeko la wagonjwa na huku mahitaji yao yakipungua, kutokana na
wingi wao, hivyo wanahitaji wasamaria wema wajitokeze kuwasaidia.
Mahitaji mengine wanayohitaji hospitalini hapo alitaja kuwa pamoja na
vifaa vya maabara navyo ni vichache,hivyo wanaomba msaada kwa
wasamaria wema na sio kuiachia serikali ambayo inamajukumu mengi.
Kwa upande wake Emmanuel Mbwiga ambaye ni Mzee wa  Kanisa la Calvary

Temple la Kilombero Jijini Arusha, akitoa msaada huo alisema mbali na
msaada huo pia kupitia vituo vyao mbalimbali wametoa msaada kwenye
vituo vya yatima vya Huruma Kwamurombo,Monduli,Esso.

Pia misaada mingine imetolewa shule za msingi Mwangaza, Olsinyai
Sombetini na Ngarenaro, lengo kubwa kusaidia watu wenye shida ili
wapate faraja nao katika kuadhimisha kilele cha kanisa hilo
kitakachofanyika Kitaifa Mbeya Julai mwaka huu.

Mbwiga alisema vitu walivyotoa maeneo hayo  ni Sabuni, ndoo za mafuta,
mchele, nguo, mahindi,daftari,soksi na vitu vingine vingi, ambavyo
vyote vina jumla ya shilingi milioni 3.

 Hata hivyo alitoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kujitokeza
kusaidia hospitali hiyo na maeneo yenye uhitaji kama vitruo vya yatima
na shuleni, ili wabarikiwe zaidi.
Mwisho