NA WAANDISHI WA UPAKO WA HABARI, ARUSHA
KUNDI la wa machinga mjini arusha leo wamevamia eneo la la
wazi lilopo
ngarenaro na kujigawia tayari kwa kufanya biashara.
Kundi hilo la
wamachinga limevamia eneo hilo ambalo lilikuwa
limezungushiwa mabati kwa
kipindi cha
muda mrefu kilichopo ngarenaro jijini hapa wakidai kuwa eneo hilo
ni la
serekali hivyo wanaenda hapo hapo kufanyia biashara maana wao wenyewe
ni
serekali tosha.
Gazeti hili la nipashe lilifika eneo la
tukio na kushughudia
wananchi hao wakiwa wanajigawia sehemu za biadhara huku
wengine wakiwa wameanza
kuchimba kwa ajili ya kujenga vibanda
vyao.
Wakiongelea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara hao
walisema
wameamua kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kukosa sehemu za
kwenda kufanyia
biashara zao kwani eneo walilopewa
la uwanja wa NMC ni lidogo haliwatoshi
wafanyabiashara wote.
Mmoja wa wafanyara
hao
aliyejitambulisha kwa jina la Emanuel mushi alisema kuwa wao
wamechukuwa
hatua hiyo kutokana na kitendo cha kukosa eneo la kufanyia
biashara katika
kiwanja cha nmc huku mkandasi ambaye
amepewa tenda hiyo
ya kuwagawia maeneo akiwa awazungusha.
Aidha alisema kuwa wameamua
kufanya au kuchukuwa hatua hii
ili serekali ijue machinga arusha hawana
mahala pa kwenda na wawaangalizie sasa
sehemu ya kuwaweka ili wafanyie
biashara zao
Alisema kuwa wamesubiri kwa muda mrefu na tangu
waambiwe
wanagawiwa eneo hilo hawajapatiwa na wamekuwa wakizungushwa tu bila
ya
mafanikio yoyote hali ambayo inawafanya wao kuishi kama
ndege.
,,leo asubuhi sisi tuliokuwa tumeweka vitu vyetu hapa nje
ya
soko la ngarenaro tumefatwa tukafukuzwa kamamaubwa kibaya zaidi
watufukuze
wakiwa wametupa sehemu ya kwenda lakini hawajatupa sehemu ya
kwenda
wanatupeleka peleka na tulivyoona hivyo na ili eneo tunaliona wazi
kila siku
tukaamua kuvamia ili tukae hapa,,alisema Mama rosemary
mollel
Waliongeza kuwa sababu ingine ya kutoka katika uwanja huo
ni
pamoja ya kuwa uwanja huo hauna miundo mbinu ya kutosha ikiemo choo
kitu
ambacho ni tatizo kubwa sana kwa afya zao.
,,unajua eneo lile ni
dogo kiukweli ni robo ya wamachinga tu
ndo wameingia katika eneo lile kibaya
zaidi askari wanaotufata kutufukuza
tukiwauliza tuende wapi wanasema mtajua
wenyewe kila tukaapo wanatufukuza
kibaya zaidi wanatuambia kuwa swali kama
hilo msiniulize maana wakati mnakuja
kutoka vijijijini kwenu hamkututaarifu
kwakua mlikuja kimnya kimnya basi
ondokeni ivyo ivyo kama ulivyokuja
,,alisema Lukas Seneu.
Machinga hao waliongeza kuwa serekali hii
imekuwa ikifanya
kazi kwa kuwakomoa kwani wanadhani kuwa machinga wengi ni
chadema hivyo
wanavyofanya hivi wanawakomoa kitu ambacho sio cha kweli na
walibainisha kuwa
viongozi hao wa serekali wanawatesa hivi ili warudi
kijijini lakini walisema
watapigana mpaka mwisho wake waone
Juhudi za
kumpat a kaimu mkurugenzi wa jiji kuzungumzia swala hili
ziligonga mwamba
kwani
ofisini hakuwepo na simu zake zote zilikuwa hazipo hewa.
No comments:
Post a Comment