BONDIA MAUGO KUPAMBANA ARUSHA 28 0CTOBER NA
KUSAKA VIPAJI
NA QUEEN LEMA,ARUSHA
Kampuni ya Mnyalu Entertiment kwa kushirikiana
na Bondia maarufu hapa nchini Mada Maugo watarajia kuibua vipaji vingi kwa
kanda ya kaskazini hususani ndani ya mkoa wa Arusha October 28 mwaka huu
ambapo pia mabondia mbalimbali watapimana uzito akiwemo yeye mwenyewe na Bondia
Gavad Zohrenvard wa Iran huku wanamichezo wengine kama vile diwani na
mfanyabishara maarufu Mjini Arusha Bw Justin Nyari naye atashiriki
Kwa mujibu wa bondia Mada Maugo alisema kuwa
Onyesho hilo ambalo litafanyika katika viwanja
vya Triple A litakuwa ni moja ya michezo ambayo mbali na kuburudisha pia
litachangia kwa kiwango kikubwa sana
hata kuibua vipaji ambapo naye diwani wa kata ya Mirerani naye atashiriki na
kiongozi yeyote wa Upinzani
Bondia Maugo alisema kuwa mpaka sasa ndani ya
mkoa wa Arusha kuna Vipaji vya hali ya juu sana lakini jambo la kushanga za mpka sasa
vipaji hivyo havijawaeza kubebwa na kuonekana hali ambayo inachangia kwa
kiwango kikubwa wapiganaji hao kupoteza vipaji
Akiongelea vipaji hivyo alisema kuwa yeye
anatarajia kucheza na bondia wa Iran ambapo mbali nay eye kucheza
pia ataweza kuwapa fursa hata wengine kutoka Arusha na kuweza kushiriki ambapo
katika kufufua Vipaji watacheza watu mbalimbali
“Mimi nitashiriki katika michuano hiyo siku hiyo
na nitapambana na bondia wa Iran lakini pia mpaka sasa na wadau wengine
akiwemo diwani wa Mererani Simanjiro naye amedhibitisha kushiriki na kuchuana
vema na mwanasiasa yeyote hasa wa upinzani nah ii itachangia kwa kiwango
kikubwa sana kuweza kuboresha na kuendelea kuibua vipaji mbalimbali kwani ndani
ya mkoa wa Arusha kuna vipaji vya hali ya juu sana”aliongeza Bw Maugo
Pia alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano
kama sita hivi ambapo ni ya utangulizi na bondia wa Arusha Robert Mroso
atapambana na bondia Selemani Tall kutoka Dar,chini ya uzito wa kilo 72 na
watacheza kwa Raundi nane na pia tuna bondia mwingine ambaye ni Abasi Ally wa
Arusha naye atapamnbana na Joseph Marwa kutoka Zanzibar chini ya uzito wa kilo
80.
Mbali na hayo alisema kuwa mabondia hao
watachuana kwa hali na mali
ambapo pia wataweza kuburudishwa na makundi mbalimbali ya wanamuziki kama vile Dogo janja,Ras Lion,John Oka, na makiundi
mengine mengi huku mgeni rasmi akiwa anatarajiwa kuwa Mzee Edward Lowasa
Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa sasa kuna
umuhimu mkubwa sana wa wadau mbalimbalui
kuhakikisha kuwa wanawekeza zaidi katika Michezo hasa kwa kuwa una hamasa kubwa
sana na unaweza kutumika kama
njia ya kuweza kuwasaidia waepukane na matizo mbalimbali ambayo yapo kwenye
jamii hasa ya ukosefu wa ajira
MWISHO
No comments:
Post a Comment