Na Bety Alex, ARUSHA
WAUMINI WACHANGA MILIONI 5 KWA AJILI YA KUONGEZA ENEO LA
KANISA,MCHUNGAJI WAO AWATAKA KAMWE WASIWE NI WATEGEMEA WAFADHILI WA NJE
MAKANISA ya leo yametakiwa kuacha tabia ya kuwategemea zaidi
wafadhili hasa katika kuchangia masuala
mbalimbali ya maendeleo ya makanisa yao kwani
hali hiyo husababisha kwa kiwango cha hali ya juu sana wafadhili hao kukomba baraka huku
wenyeji wakiwa hawana baraka kutoka kwa Mungu.
Ni vizuri kama wakristo wao wenyewe wakawa ni wafadhili na
kama watajijengea tabiaya kujichangia wao wenyewe basi kwa kiwango cha hali ya
juu sana
watasababisha hata kizazi cha watoto wao kukua katika msingi wa imani ambao
unawataka wao wenyewe waweze kujitegemea zaidi
Kauli hiyo imetyolewa na Mchungaji Elinaisha Ayo wa kanisa la
FPCT Sombetini Mkoani hapa wakati akiongea katika harambee ya kuchangia ujenzi
wa kanisa hilo
mapema Wiki iliyopita ambapo pia ibada hiyo ya Harambee ilienda sambamba na
Mahubiri ya kukataa kuwa tegemezi kwa wafadhili wa nje
Mchungaji huyo alisema kuwa ni vizuri sana
kama Wakristo wakahakikisha kuwa wanaaachana na tabia ya kuwawazia wafadhili
kuja kuwapa msaada ilihali wao wanaweza kujichangia na kama
makanisa yataendelea kuwategemea zaidi wafadhili ni wazi kuwa hata kizazi
kijacho nacho kitakuwa ni kizazi tegemezi zadii
Alisema kuwa kama wakristo wakiwa na Umoja wataweza
kuchangia maendeleo ya makanisa yao na hivyo hali
hiyo itafanya hata kazi ya injili kuwa raisi sana na hivyo hata wale ambao wanachangia
huduma mbalimbali nao wataweza kupata baraka tofauti na pale ambapo wafadhili
wanatoka nje ya nchi na kuja kusaidia makanisa
“leo unakuta kanisa lina uhitaji ili liweze kufanikisha
zoezi hilo linawafikiria zaidi wafadhili na kama maandiko yanavyosema ni kuwa
kila atakayefanya kazi ya bwana kwa umakini na kwa moyo ndiyon atakaye barikiwa
sasa hapa hawa wafadhili wote wataondoka na baraka na sisi tutabaki kama
tulivyo tuache kufikiria kusaidiwa bali tufikirie zaidi jinsi ya kujisaidia
sisi wenyewe’aliongeza mchungaji Elinaisha
Pia aliongeza kuwa kama makanisa ya leo yatakuwa na desturi
ya kujichangia basi hata watoto wadogo nao watakuwa na moyo wa kuweza kuchangia
kwa kiwango kikubwa kazi mbalimbali za injili ambapo hata kwa kizazi chao nacho
kitakuwa na Utoaji mzuri sana tofauti na pale ambapo wazazi na walezi
wanapowafikiria sana wafadhili kuja kuwasadia
“Tunachokipanda ndicho kitakachokivuna na kama tukipanda
mbegu bora ndio itakayoweza kuwasaidia hawa watoto wetu kwa maana hiyo basi
kuanzia sasa tunaanza kujiopanga ndani ya makanisa yetu hasa hapa Sombetini na
watoto nao wawe ni wachangiaji hasa wa harambee kama
hizi kwa manufaa ya hapo baadaye”aliongeza Mchungaji Elinaisha
Akiongelea harambee hiyo ambayo ilifanyika kanisani hapo
alisema kuwa Wakristo wa kanisa hilo
wamefanikiwa kuchanga kiasi cha zaidi ya milioni tano ambazo zitatumika kwa
ajili ya kupanua eneo la Kanisa hilo huku lengo
halisi likiwa ni kueneza Injili ndani ya eneo hilo la Sombetini na Mkoa wa Arusha kwa
ujumla
MWISHO
No comments:
Post a Comment