Na Bety Alex, Arusha
Waziri Agrey Mwandri amewataka wakristo kuachana na tabia ya
kukwepa kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo vinaongeza maarifa ya kiroho na
kimwili kwani kwa njia ya vitabu hata maarifa juu ya ufalme wa Mungu nayo
yanaongezeka sana
Mwandri aliyasema hayo wiki iliyopita katika kanisa la Winner
Chapel Intrenational Arusha lililopo maeneo ya Kaloleni Mjini hapa wakati
akizindua rasmi Kitabu kilichoandaliwa na Muinjilisti Paul Dickson
kijulikanacho kama Ufalmwe wa Mungu hutekwa na
wenye nguvu.
Alisema,kwa sasa wapo baadhi ya wakristo ambao wanapenda
kujisomea vitabu ambavuyo havina maslahi na Mungu na badala yake vitabu hivyo
vinahamsisha dhambi jambo ambalo kwa sasa wanatakiwa kulikataa
Alifafanua kuwa kama kila mkristo atahakikisha kuwa hapotezi
muda wake mwingi kwenye vitabu hivyo a,mbavyo havijengi basi ni wazi kuwa hta
dhambi ndani ya mkoa wa Arusha lakini Tanzania kwa ujmla nazo zitapungua
kwa kiwango
Alibainisha kuwa kwa kusoma vitabu ambavyo vina madharai ya
mwenendo wa Kimungu kunasaidia sana
kuhimiza hata nguvu za Mungu kushuka na kuongoza katika mambo mbalimbali.
“jamani jiwekeeni utaratibu wa kuhakikisha kuwa mnasoma vitabu
venye madhari ya Kimungu msinione hapa napambana kweli kule Bungeni lakini
niwaambieni kuwa muda wangu mimi natumia hivi hivi vitabu vya mungu kujisomea
na kuhakikisha kuwa naktafuta hata suluhu kule Bungeni hivyo basi igeni mfano
huu “aliongeza Mwandri
Katika hatua nyingine Mwandishi wa kitabu hicho ambaye ni
Muinjilisti Paul Dickson alisema kuwa lengo na maudhui ya kitabu hicho
kijulikanacho kama Ufalme wa Mungu hutekwa na
wenye nguvu, kina malengo ya kuhakikisha kuwa kinawakomboa baadhi ya watu
katika ufalme wa Mungu
Muinjlisti huyo alidai kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu
ambao wanatamani sana kuwa na falme wa Mungu
lakini bado hawajaju hata siri za kuweza kuuteka ufalme huo hali ambayo wakati
mwingine inasababisha waone kama ni wakosaji
“hiki kitabu kina siri nyingi sana za uponyaji na jinsi ya
kuuteka ufalme wa Mungu hivyo basi natamani kuona kuwa watuw a sasa hususani
mkoa wa Arusha na Tanzania wanaweza kuinuka
na kutoka katika hali Fulani hata za umaskini kwa kuwa ufalme wa Mungu
kuuteka ni bure kabisa’aliongeza muinjilisti huyo
Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa vitabu vya Mungu
vinaweza hata kuokoa lakini bado ipo changamoto kubwa sana
kwa waaandishi wa vitabu kwa kuwa baadhi yao
huandika zaidi vitabu ambavyo vinahusu mapenzi na kusahau vitabu vya kuwakomboa
watu jambo ambalo si jema kwa maendeleo ya watu
MWISHO
No comments:
Post a Comment