KAMPENI ZA CHADEMA KWA KATA ZA DARAJA MBILI NA BANGATA
KUANZA OCTOBER 3
Na Mery Kitosio, ARUSHA
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kinatarajia
kuanza rasmi kampeni zake katika kata za daraja mbili manispaa ya Arusha na kata ya Bangata Wilayani Meru mkoani Arusha
ambapo kampeni hizo zinatarajiwa kuwa kuanza rasmi October tatu na kuongozwa na
ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Goodbles Lema na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari
Hayo yamelezwa mjini hapa na Katibu wa mkoa wa chama hicho Amani Golugwa jana ambapo alisema kuwa mpaka
sasa wameshafanikiwa kupata wagombea watakosimama katika kinyanganyiro hicho
ambacho kitahusisha vyama mbalimbali vya siasa kwa mkoa wa Arusha.
Golugwa alisema kuwa ndani ya chama hicho wamesharidhia
wagombea wawili kuweza kusimama ambao ni bw Prosper Msofe ambaye atasimama kama
mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika kata ya daraja mbili huku kata ya
Bangata Meru nayo ikiwakilishwa na Erick Samsoni ambapo pia kampeni za kuchukua
kata hizo nazo zitaendeshwa kwa njia ya kitaalamu na kidemokrasia sana.
“hawa watu wawili mpaka sasa chama kimeshawapa baraka zote
za kuweza kugombea kwa kata hizi mbili lakini kwa sasa tunatarajia kuhakikisha
kuwa kamwe demokrasia ya watanzania haibakwi na baadhi ya viongozi walafi na
badala yake tutahakikisha kuwa kila mtu anatumia vema demokrasia yake ili
kupata haki zake za msingi”aliongeza Golugwa
Hataivyo aliongeza kuwa ndani ya kampeni hizo ambazo
zinatarajiwa kuanza wiki ijayo chama hicho kamwe hakitamvumilia kiongozi yoyote
yule ambaye atakuwa anatoa Rushwa ya aina mbalimbali zikiwemo Rushwa za kutumia
magari ya Serikali ndani ya kampeni na badala yake kiongozi atakayefanya hivyo watamuhisha
na Rushwa na hivyo chama hicho kitasimamia ukweli kwa kuwafikisha ndani ya
Magareza
Awali alisema kuwa mbali na kuanza rasmi kampeni kwa kata za
Daraja mbili na Bangata pia chama hicho kimelazimikka kuwapa waraka muhimu
chama cha Wananchi Cuf juu ya mapungufu mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea
katika mji wa Arusha hasa katika harakati zao za mikutano ya Hadhara ambayo
inaendelea ndani ya Mji wa Arusha
Golugwa alisema kuwa chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko
kadhaa baadhi ya wanachama wa Chadema
wamewafanyia vurugu huku vurugu hizo zikihusishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo
la Arusha Mjini bw Goodbless Lema hali ambayo inasababisha muendelezo wa Siasa
chafu ambazo ndizo chanzo kikubwa sana cha ubakaji wa Demokrasia hadharani.
“Sisi kamwe hatuwezi kuwafanyia hawa Cuf vurugu kwa kuwa
tunajua kuwa hilo ni suala la uvuinjifu wa amani ndani ya nchi yetu na kwa
maana hiyo tunapenda kuwaambia kuwa tunawapenda na pia tunawakaribisha ndani ya
mji wa Arusha ila wasitafute visngizio vya hapa na pale ila watafute hoja
ambazo zinajenga na kuimarisha hata Maslahi ya Nchi”alibainisha Golugwa
Mbali na hilo katibu huyo pia alisema kuwa Cuf inatakiwa
kuhakikisha kuwa inakuwa na Matamko ambayo yanalenga kumkomboa Mtanzania na
wala sio kuwa na matamko ambayo hayana tija mbele za jamii kama ambavyo wamefanya
kupitia Kwa Naibu Mkurugenzi wa habari
uenezi na haki za binadamu, Abdul Kambaya ambaye alitoa matamko ambalo lilikuwa
na matisho na lugha isiyofaa kwa nchi na jamii za kitanzania
MWISHO
No comments:
Post a Comment