NHC ARUSHA YAFANIKIWA KUJENGA NYUMBA 100 ZENYE THAMANI YA
BILIONI SITA HUKU KATI YA NYUMBA HIZO 30 ZIKITUMIKA KAMA NYUMBA ZA DHARURA
Na Queen Lema,ARUSHA
SHIRIKA la Taifa la Nyumba hapa nchini (NHC)limefanikiwa
kumaliza kujenga mradi wa nyumba 100 zenye garama ya zaidi ya Bilioni sita
ambapo nyumba hizo zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kutumika kama makazi
bora hasa kwa watumiaji mbalimbali wa nyumba wa shirika hilo ambao watahamishwa
ili kupisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya shirika hilo
Akiongea jana mara baada ya kuzindua Mradi huo uliopo kwenye
eneo la Levolosi Mjini hapa Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara katika shirika hilo Bw David Shambe
alisema kuwa ujenzi wa mradi huo umedumu kwa muda wa mwaka mmoja
Aliongeza kuwa kupitia mradi huo wa nyumbautakuwa ni wa
tofauti sana na miradi mingine kwani mradi huo
pia utaweza kuwanufaisha hata wale ambao wanahamishwa kwa haraka katika nyumba
mbalimbali za shirika hilo
ili kupisha ujenzi wa miradi mbalimbali
Alifafanua kuwa mradi huo wa nyumba 100 kwa sasa utaweza
kuuzwa nyumba 70 huku nyumba 30 zilizobakia zitatumika kama nyumba za dharura
na hali hiyo itaweza kuwasaidia watanzania ambao wanahamishwa huku wakiwa
hawana makazi ya kusihi kwa haraka sana
“huu mradi utakuwa ni wa tofauti sana kwani mradi huu
umejiwekezaa hata kwa ajili ya masuala mbalimbali ya dharura tofauti na miradi
mingine na kwa hali hiyo utaweza kuokoa maisha ya watanzania walio wengi sana
ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kuwataka kuhama na kupisha
ujenzi kwa haraka kwani wengi wao wanaposikia hali kama hizo wanajikuta wakiwa
katika wakati mgumu sana”aliongeza Bw David
Mbali na hayo alisema kuwa shirika hilo limedhamiria kujenga
nyumba bora na za kisasa zaidi ambazo zitaweza kuwanufaisha wananchi wote hasa
wale ambao wapo pembezoni mwa miji na majiji mbalimbali ndani ya nchi ya
Tanzania ingawaje kwa sasa kuna changamoto kubwa sana ya uhaba wa Ardhi za
kujengea nyumba za kisasa ili kuwa na makazi bora na yenye viwango vya hali ya
juu sana
Alibainisha kuwa changamoto hiyo ya Ardhi kama itaweza
kutatulika kupitia Halmashauri basi itaweza kuongeza idadi hata ya nyumba
bora na
za kisasa tofauti na sasa ambapo kuna uhaba mkubwa sana wa Ardhi kwa
ajili ya kujengea makazi bora nay a
kisasa zaidi.
Katika hatua nyingine alisema kuwa ili kujenga nyumba za
viwango tofauti tofauti Shirika hilo kwa sasa lina mipango na mikakati
mbalimbali ya kujenga nyumba bora na za kisasa hasa kwa wenye vipato vya chini
ambapo watajenga nyumba 223 katika mkoa wa Dar es saalam na nyumba hizo zitawajumuisha
wale wote wenye kipato cha chini sana.
“Moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunajenga nyumba
elfu kumi na tano lakini kwa sasa hizi nyumba za bei ya chini kwa watu wenye
kipato kidogo wataweza kunufaika nazo na baada ya kumaliza kwa Dar es saalam
baadaye tutaenda mahala pengine kwani hii nayo itachangia sana kuweza kuepusha
jamii na makazi holela ndani ya jamii zetu”aliongeza Bw David.
MWISHO
No comments:
Post a Comment