baadhi ya watendaji wa wa wizara ya afya wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mery Kitosio,MERU
VIONGOZI mbalimbali hasa ngazi za Vijiji na Kata Wilayani
Meru mkoani hapa wametakiwa kuhakikisha
kuwa wanasimamia vema sera za wazee ambapo kwa sasa Halmashauri hiyo inahudumia
huduma za afya bure wazee wote wenye umri wa miaka 60.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw
Goodson Majola wakati akiongea katika kikao cha baraza la madiwani(FULL
COUNCIL) mapema jana wilayani humo.
Aidha Bw Majola alisema kuwa kwa sasa halmashauri hiyo imeaanza
rasmi mpango mkakati wa kutekeleza sera za wazee ambao wana umri wa zaidi ya
miaka 60 na kwa hali hiyo ni jukumu la kila
kiongozi kuhakikisha kuwa wazee wanapata huduma bora za afya
Pia alisema kuwa ili zoezi hilo
liweze kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu viongozi hao wa Kata wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanakuwa na idadi ya wazee ambao wapo katika jamii zao ambapo
pia hali hiyo itaweza kuwasaidia kwa kiwango kikubwa sana.
“kwa kiongozi ambaye hatausika na kuwasaidia hawa wazee
katika kupata haki zao za msingi au kuwapa garama hawa wazeee basi sisi
tutahakikisha kuwa tunawachukulia hatua kali na za kisheria kwani ni
tunachikiitaji ni kuhakikisha kuwa kila mzee hapa Meru anapata haki matibabu bure
kabisa”aliongeza bw Majola
Awali alibainisha kuwa mpango huo ni endelevu sana kwa Halmashauri hiyo
ambapo kwa sasa wana mpango wa kuhakikisha kuwa Sera zote ambazo zipo chini ya
Wizara mbalimbali zinatekelezwa tena kwa wakati kwani uwezo wa kutekeleza sera
hizo upo ingawaje mara nyingine sera hizo zinaachwa huku wananchi nao wakiwa
wanapata taabu katika shuguli za kila siku..
“Ni Muhiumu sana kwa kila sera kutekelezwa kwa kiwango cha
juu sana kwani kukwepesha sera mbalimbali za kijamii ndio chanzo cha matatizo
makubwa sana kwenye taifa la leo na kwa maana hiyo kila Sera itatekelezwa tena
kwa wakati kwani ni haki ya jamii kupata huduma zitokanazo na Halmashauri zetu
kama ilivyo sera ya wazee kwa sasa”aliongeza Bw Majola.
Hataivyo viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Meru walisema kuwa
kama Sera hiyo itatekelezwa basi itaweza kupunguza matatizo mbalimbali ambapo kwa sasa hata wengine wanashindwa kujua na kutambua kuwa
wazee wote wanatakiwa kupewa matibabu bure kwani Tayari Serikali imeshaona
umuhimu huo kutokana na hali halisi na magonjwa amnbayo yanawakabili wazee
wengi kwa sasa
Wazee hao walibainisha kuwa mbali na Halmashauri hiyo kuanza
kutangaza kuwa wanawapa bure wazee huduma za afya pia nao watumishi wa afya
wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wazee nao wanapaswa kuhudumiwa vema
pasipokuwa na masumango ya aina yoyote kwani zipo baadhi ya hospitali ambazo
zinawanyanyasa sana
wazee hasa wenye magonjwa nyemelezi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment