KIFO CHA BABA MZAZI WA TUNDU LISU,NA ALUTE
MUGWAI AMBAYE NI MAWAKILI KATIKA KESI YA LEMA CHASABABISHA KESI KUHARISHWA
Kesi ya Rufaa iliyokuwa inamkabili Mbunge wa
Jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema imeharishwa mpaka October 2 kutokana na
Mawakili wawili ambao ni Alute Mugwai na Tundu Lisu kufiiwa na baba yao mzazi na mazishi
kufanyika Kesho kutwa
Kesi hiyo ya Rufaa ambayo inaendeshwa na Majaji
watatu ambao ni Othaman Chande,Natalia Kimaro,na Salum Masati pia
mahakama imeamuru baadhi ya walengwa kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu
zote ili kesi hiyo iweze kusikilizwa
Aidha ilidaiwa mahakani hapo mbele ya Jaji Mkuu
Othaman Chande ambaye alitoa ufafanuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake alidai
kuwa kesi hiyo itasikilizwa October 2 ambapo Wajibu rufaa nao wanatakiwa
kuhakikisha kuwa walete hoja zao zote ili kuraisisha masuala mbalimbali ndani
ya kesi hiyo ya Mbunge wa Arusha Mjini
“hawa mawakili ambao ni ndugu na wapo pande
zote mbili ni ndugu na kwa maana hiyo wamempoteza baba yao mzazi kwa hali hiyo
watamzika siku ya Jumamosi lakini pamoja na hayo yote taratibu mbalimbali nazo
zinazohusu hii kesi zinatakiwa kuboreshwa na kuwasilishwa hapa October 2 mwaka
huu nah ii ni kwa wahusika wote”aliongeza Jaji Chande
Hataivyo Jaji huyo aliamuru mahakama
kuhakikisha kuwa Mahakama ihakikishe kuwa wajibu rufaa wawasilishe hoja zao za
awali kabla ya September 26 mwaka huu,huku naye muomba Rufaa na
Mwanasheria wa Serikali naye anatakiwa kuhakikisha kuwa wanaleta majibu kabla
ya September 29.
Katika hatua nyingine ilidaiwa mahakamani hapo
naye Mwanasheria wa upande wa walamikaji wa naye alete hoja zake kuhusu
rufaa kabla ya September 28 ili kuweza kuruhusu kesi hiyo kusikilizwa kwa
uraisi hapo October 2 ndani ya Mahakama hiyo.
Hataivyo kwa upande wa mawakili wa Serikali
atawakilishwa na wakili Timothy Vitalisi ambapo kwa upande wa Majaji
wataongozwa na Jaji Othmani Chande
Katika hatua nyingine mara baada ya Kesi hiyo
kuharishwa mamia ya wananchi wa mji wa Arusha walilazimika kutembea miguu na
kufunga baaadhi ya barabarani za mji wa Arusha kutoka katika eneo hilo la mahakama hadi
kufikia katika Ofisi za chama hicho zilizopo katika eneo la Makao Mapya.
MWISHO
No comments:
Post a Comment