MUINJILISTI WA EAGT ATUMIA MSTARI WA ZAKARIA 4.6 KATIKA
UCHAGUZI WA UVCCM NA AIBUKA MSHINDI KAMA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA MANISPAA
YA ARUSHA
Na Be ty Alex, ARUSHA
MUINJILISTI wa kanisa la EAGT Sinoni mjini hapa amefanikiwa
kushinda kinyanganyiro cha mwenyekiti wa umoja wa Vijana (UVCCM)na kuweza
kuweka historia kuwa hata viongozi mbalimbali ndani ya makanisa wana nafasi
kubwa sana ya
lkushiriki chaguzi mbalimbali ndani ya Nchi
Akiongea na nyakati mara baada ya kushinda mwenyekiti huyo
ambaye ni Martin Munisi alisema kuwa ameamua kushiriki katika chaguzi hizo
kwani bado kuna uwezekano mkubwa sana
hata watu wanaomjua Mungu kuweza kuchukua nafasi ya uongozi
Bw Martin alieleza kuwa hapo awali alilazimika kutumia
biblia ambayo ina mistari imara na kuweza kuomba nafasi kwenye chama hicho
ambapo alipinzana na watu wengi ambao walikuwa wanaonekana kama wana uwezo
mkubwa sana
lakini baadaye Mungu alimtetea zaidi
“Unajua wartu wengi sana wanaogopa Siasa lakini kama sisi
ambao tunajua kweli ya mungu tutafanya siasa tutaweza kuokoa walio wengi zaidi
kwani tutaweza kuhubiri kweli na kweli hiyo ikaweza kuwaweka watu huru tofauti
na pale watu wa mungu watakapokuwa wanaogopa siasa na huu ni muda mzuri sana
kwa Kanisa kusimama na kutafuta nafasi mbalimbali za uongozi wan chi”aliongeza
bw Martin
Alifafanua kuwa lengo
halisi la kugombea ilihali yeye ni muinjilisti ni kuhakikisha kuwa anawavutia
hata watu wengine nafasi ya kugombea huku wakiwa wanamjua Mungu na kutokana na
hili wataweza kufanya asilimia kubwa sana ya Viongozi kujikwepa na dhambi
ambayo ni tishio kubwa sana.
Aliendelea kusema kuwa kwa watu ambao wanamjua Mungu wana
uwezo mkubwa sana wa kuweza kupata nafasi za
uongozi kwani Muongozo mzuri ni biblia na sasa bado kuna changamoto kubwa sana katika kutetea haki za taifa la Tanzania ya leo
Alibainisha kuwaendapo kama wana wa Mungu watajitokeza kwa
wingi basi watasaidia kuwapa changamoto ya kufanya hata vema baadhi ya viongozi
ambao wapo maldarakani lakini wanatumia vibaya nafasi zao za uongozi hali
ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana
madhara ya Umaskini, na Umwagaji wa damu ambazo hazina hatia mbele ya macho ya
Mungu
“Nawasihi sana watu wa mungu
kuhakikisha kuwa pindi mpapokweda kugombea mtumie Biblia na imani zenu ziwe juu
tukiwa wengi ambao tunamjua Mungu itaweza kutusaidia sana sisi kuweza kupata nafasi ya kupambana
na maadui mbalimbali ambao ndio chanzo cha kuyumba kwa maisha ya mtanzania
kwani mimi nilitumia kitabu cha Zakaria 4.6 na nikapata ambacho
ninakipata”aliongeza Bw Martin
Pia alisema kuwa ili kufanikisha kazi ya Mungu na siasa ana
mikakati mbalimbali yan kuhakikisha kuwa Vijana wa kitanzania hususani wa mkoa
wa Arusha wanainuka Kiimani sanjari na kuongeza na kuimarisha chama cha kuweka
na kukopa ili waweze kujikwamua kimaisha kwani wengi wao hawana hata mitaji ya
kujiendesha wao kwa wao.
MWISHO
No comments:
Post a Comment