Na Queen Lema,ARUSHA
ASKOFU HOTAY WA KANISA LA ANGILIKANA DAYOSISI YA MOUNT KILIMANJARO AKABIDHIWA RASMI KITI CHA UASKOFU
WALIOSABABISHA NA KUFUNGUA KESI WASAMEHEWA MBELE YA KANISA
WAKATI zikiwa zimepita siku chache mara baada ya Mahakama
kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali pingamizi la waumini wa kanisa la
Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro juu ya Uaskofu wa Askofu wa kanisa
hilo Stanley Hotay jana(Leo)kanisa hilo limemuweka rasmi kazini askofu huyo
sanjari na kutangaza msamahaa kwa waumini hao watatu kwani wamechangia sana
kanisa hilo kupoteza muda kwenye kesi hiyo pamoja na aibu kubwa kwenye masikio
ya watu wengi
Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya
kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo
la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka sasa
wameshatangaza Msamaha kwa watu hao
ambao walitia aibu kanisa hilo
hivi karibuni
Askofu huyo alisema kuwa hapo awali baadhi ya waumini
akiwemo yeye mwenyewe walikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na kesi hiyo lakini kutokana na ukweli na
haki ya Askofu Hotay aliweza kupata haki
yake kupitia mahakama Septembe tano mwaka huu huku waliofungua kesi hiyo
wakishinndwa kusonga mbele
“wakati Kesi hii inaanza mimi nilikuwa katika wakati mgumu
sana kwani nilikuwa na Presha ambayo wakati mwingine ilinipelekea hata
kushindwa kuona na huku kwa upande wa Askofu Hotay naye alishindwa kukaa kwa
amani lakini kila mara saa nyingine alikuwa anahitajika hata kwenda
mahakamani lakini kwa sasa kweli ya
Mungu imejulikana na imeonekana mahakamani wiki iliyopita”aliongeza Dkt Mokiwa
Mbali na hayo alisema kuwa kuna masaa mengi sana ambayo
yamepotea katika Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na waumini watatu lakini kanisa
kama kanisa linapswa kuhakikisha kuwa linatoa msamaha wa kweli ambao unatoka
ndani ya Mioyo yao kwani watu hao walidanganywa na hata kufikia hatua ya kutoka
nje ya Kundi bila kujua kuwa hali hiyo inachangia sana hata mmonyoko wa Kanisa
na aibu sana
“kwa kweli hawa watu wametupa aibu ya hali ya juu sana
lakini tunapswa kuhakikisha kuw tunawasamehe hawa watu kwani walikuwa hawajui
wafanyalo ingawaje si hawa waumini watatu pekee yao bali ni nyuma yao kulikuwa
na watu wengi sana ambao hata wengine nao walichangia kwa kuwapa fedha za
kwenda kufungulia kesi na wao pia tumewasamehe wote kabisa na kanisa
lihakikishe kuwa linawaombea Toba na kuwapenda sana”aliongeza Dkt Mokiwa
Katika hatua nyingine alisema kuwa kanisa hilo limempa
Nafasi ya kuongoza jimbo hilo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo na kutokana
na hali hiyo kiti hicho ambacho alikuwa hakitumii kutokana na kesi ambayo ipo
mahakamani sasa anaanza kazi rasmi kwa kuwa sheria inamruhusu huku waumini
wa kanisa hilo nao wanatakiwa kumpa
ushirikiano na kukumbuka Viapo mbalimbali ambavyo vinatumika na kanisa hilo
Naye Askofu Stanley Hotay aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa ili ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe kuwa
unatoa msamaha hata kwa wale ambao
wamekuwa ni vikwazo vya kushindwa kufikia katika malengo mbalimbali ambayo
yanatakiwa kufikiwa ingawaje vikwazo ni vingi sana katika safari ya Ushindi
Askofu huyo alifafanua kuwa pamoja na kuwa amepita katika
wakati mgumu sana hasa wa kuwa na kesi ya
kutotambulika na waumini wake lakini bado ana nafasi kubwa sana
ya kuweza kuwatumikia hao hao na kuwafanya wabadilishe fikra kwani hapo awali
hawakujua wanachokifanya hali ambayo ilizaa aibu kubwa sana mbele ya kanisa la Angilikana dayosisi
ya Mout Kilimanjaro.
“ingawaje mimi nilipita katika wakati mgumu sana lakini wao
walikuwa ni zaidi sana kwani mtu akijiaanda kukupiga ngumi kubwa yeye ndiye
anayetumia nguvu nyingi sana kuliko yule ambaye anatarajia kupigwa na mimi
nataka kuwaambia kuwa wapo huru kabisa dhidi yangu na bado mimi nawatambua kama
wanakondoo wangu”aliongeza Askofu Hotayi
Aliwataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanasahau
hilo na kuanza kufikiria upaya kwani bado kanisa hilo lina muitikio mkubwa sana
wa kuweza kuwasaidia waumini pamoja na jamii kwa kuweza kuhamasisha maendeleo
ambayo ndiyo yana amani kwa maslahi ya Taifa la Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ambaye alikuwa ni
mgeni rasmi katika ukabidhiwaji wa kiti hicho kwa askofu huyo ambaye hapo awali
alikuwa ameshasimikwa kama askofu wa kanisa hilo alisema kuwa wakristo
wanatakiwa kujua hakuna dhambi mbaya sana kama dhambi ya kutamani madaraka
kwani dhambi hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa migogoro
sana
Bw Mulongo aliongeza kuwa ni vema kama mtu anayetamani
Madaraka hata kama ni ya Uaskofu basi kuomba Mungu kna wala sio kuwa chanzo cha
kuanzisha Kesi ambazo hazina Tija na ambazo zinapotosha hata maana halisi ya
Wokovu huku tamaa kama hizo zikiwa ni chanzo
pekee cha kuweza kusababisha amani kutoweka
MWISHO
No comments:
Post a Comment