na gladness
mushi,arusha
Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia,January Makamba amesema kuwa taasisi za dini hapa chini zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na kuisaidia serikali kwa kutoa ufadhili mbalimbali wa elimu kwa jamii yenye uhitaji pamoja na kuhubili amani.
Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia,January Makamba amesema kuwa taasisi za dini hapa chini zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na kuisaidia serikali kwa kutoa ufadhili mbalimbali wa elimu kwa jamii yenye uhitaji pamoja na kuhubili amani.
Makamba
aliyasema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za kidini na
utamaduni zinazoadhimishwa kila mwaka na dhehebu la dini ya wahindu wa jamii ya
kilala kutoka jimbo la kusini nchini India,ambao wanaasili ya kiasia
waishio hapa nchini, kwa kutoa shukrani wakati wa mavuno .
Alisema kuwa sherehe hiyo
inamanufaa makubwa hapa nchini katika kuwaunganisha watanzania kiutamaduni
,kiimani na wenzao wanaotoka madhehebu ulimwenguni katika kudunisha
amani,ambapo alieleza kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa taasisi za dini
hapa nchini,itaendelea kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo kwenye vifaa
mbali mbali vinavyokuwa na manufaa kwa wananchi ili kuweza kuwasogezea
maendeleo.
Aidha
alizihakikishia taasisi hizo kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa
karibu ikiwa ni pamoja na kuheshimu imani ya kila dhehebu bila kuingilia na
kuzitaka taasisi hizo kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani
kupitia Nyanja mbalimbali .
Naye msemaji wa
chama cha Arusha Meru Maalayelee Assiociation(AMMA),Prem Cheriam alisema kuwa
AMMA imeanzishwa hapa nchini miaka 6 iliyopita ikiwa na lengo la kuwaunganisha
waumini wa dini hiyo ya wahindu na wenzao waishio hapa nchini na nje ya
nchi.
Alisema lengo la
ni kumshukuru mungu kwa kutoa sehemu ya mavuno yao kwa kuisaidia jamii kama
shukrani yao kwa mwenyezi mungu kwa kufoa sadaka na kwamba mwaka huu wameamua
kusaidia katika Nyanja ya elimu kwa kufadhili wanafunzi 7 kusoma masomo ya
kompyuta nje na ndani ya nchini.
Prem alisema
kuwa mpango huo utawanufaisha zaidi wanafunzi wasio na uwezo ambao wanalelewa
kwenye vituo vya watoto yatima na kwamba AMMA imeahidi kujenga
bwawa moja kwenye shule moja wapo ya msingi katika jiji la Arusha
litakalosaidia kuwaimarisha vijana kimichezo ya kuogelea .
Katika sherehe hizo watu mbalimbali
walihudhuria wakiwemo wabunge wa Mikoa ya Arusha na Manyara na viongozi wa
ngazi mbali mbali serikalini pamoja na wenzao wa jamii hiyo kutoka mataifa
mbalimbali na kwamba sherehe hizo zilipambwa na kunakshiwa na vikundi
mbalimbali vya utamaduni na sanaa kutoka Nchi ya India .
Mwisho
No comments:
Post a Comment