Serikali imetenga sh.bilioni 9.8 kwa ajili ya mikopo ya vifaa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuboresha uchimbaji wao na watakopeshwa kupitia vikundi watakavyojiunga na itakuwa mkopo endelevu ili kuinua sekta hiyo ya madini kupitia wachimbaji hao.
Hayo yalisemwa leo na Kamishna wa madini wa kanda ya kaskazini Eng.Benjamini Mchwampaka wakati wa mahojiano na waaandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko mkoani arusha.
Alisema kuwa kupitia mikopo hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa wachimbaji hao kupata vifaaa hivyo ili kuweza kuinua uchimbaji wao na kuwa wa kisasa zaidi ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini ambapo hivi sasa wamekuwa wakikwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa hali ambayo wanachimba ila hawapati madini ya kutosha.
Ameongeza kuwa wachimbaji
wadogo wa kanda ya kaskazini bado wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika uzalishaji madini ikiwemo kutokuwa na vifaa
vya uchimbnaji vya kisasa ,bei kubwa ya milipuko na elimu ndogo ya
uchimbaji madini hayo hali ambayo inakwamisha jitihada zao za
kuchimba madini hayo na kuwarudisha nyuma katika kujikwamua kiuchumi
.
Alisema kuwa hivi sasa
wachimbaji wadogo walio wengi wanachimba kwa mazoea na vifaa duni ambapo
elimu ya utambuzi madini sehemu yalipo ni ndogo hali ambayo inasababisha
kutopata madini yakutosha na kutumia gharama kubwa zaidi.
Eng.Mchwampaka alisema kuwa
katika kanda hii wachimbaji wamekuwa wakichimba kiholela bila lessen hali
ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na hata kusababisha kifo
na madhara mbalimbali ambapo maeneo hayo yanachimbwa kwa kesi
sana hali ambayo ni hatari kwa badala yake wachimbaji wafate
taratibu za kuchimba eneo tengefu kwa madini kwa maendeleo yao na usalama
wa maisha yao kuepuka kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Aidha aliongeza kuwa hivi sasa
ofisi ya kanda imejiwekea mkakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma
karibu na wachimbaji katika kanda hii hususan kutoa elimu ,ya uchimbaji
wa madini kitaalamu zaidi,hali ya masoko ,afya migodini ,ajira na
kutoa mafunzo kwa vitendo ya namna ya ulipuaji mogodini sambamba na
watatoa fursa ya namna ya uchimbaji salama na wenye tija na maendeleo kwa
maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Eng.Mchwampakka alisema kuwa
hivi sasa wako kwenye mchakato wa kuandaa maonyesho ya vito ,na madini
mbalimbali yatakayofanyika oktoba 28 hadi 30 mwaka huu mkoani hapa ambapo watahiusisha wafanyabiashara wote
ncnini na nchi jiran ikiwemo Kenya ,DRC kongo ,Zambia ,Madagascar ,Malawi
,Ethiopia ,Afrika ya kusini na Msumbiji ili kuweza kubadilishana uzoefu
na kuweza kuongeza ushindani katika sekta ya madini nchini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment