WATUMIENI MAAFISA VIJANA MUEPUKANE NA KERO ZA VIJANA
MITAANI- DKT FENELA
Na Queen Lema, Arusha
WAZIRI wa
habari,michezo na Utamaduni,Dkt Fenela Mkangara amezitaka Halmashauri zote ndani
ya mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa zinajiwekea utaratibu wa kuwa na maafisa
Vijana kwa kuwa kama wataweza kufanya hivyo basi watachangia kwa kiwango
kikubwa sana
kuweza kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili vijana
Zipo Halamshauri ambazo zinakabiliwa na masuala ya
changamoto za Vijana lakini hakuna afisa yoyote ambaye ana uwezo wa kutatua kero za vijana hivyo
asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa
wanalalamika ovyo juu ya Serikali
Waziri huyo aliyasema hayo Jana Jijini hapa wakati akiongea
na viongozi mbalimbali wa Jiji la Arusha akiwemo Mkuu wa Wilaya kuhusiana na
maendeleo ya Vijana pamoja na changamoto,utatuzi wake kwa kipindi miaka
iliyopita.
Dkt Fenala alisema kuwa endapo kama Hallkmashauri zote za
Jiji la Arusha zitaweza kuwatumia vema hao maafisa Vijana basi zitachangia sana maendeleo ya Vijana
kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana wa sasa wanabaki wakiwa wanalamikia
Serikali kwa kushindwa kuwajua na
kuwatambua jambo ambalo si la kweli
Alisema kuwa kupitia Maafisa Vijana hao ambao wataweza
kutatua changamoto ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya vijana
lakini kwa kuwa kwa sasa hakuna maafisa
hao basi Halmashauri zinasema kuwa zinawasaidia vijana huku mitaani vijana bado
wakiwa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana.
“Wizara yangu imeweka mikakati ya kuondoa matatizo ya vijana
lakini halmashauri pekee haziwezi hii kazi ni nzito jamani ni lazima mtekeleze
ahadi Raisi ya kuwa na maafisa Vijana ambao wataweza kutukusanyia hawa vijana
na kisha hata kama tunakitu cha kuwapa tuweze kuwapata kwa ukaribu sana na pia hii itasaidia sana vijana hawa waache kulalamika
ovyo:”aliongeza Dkt Fenela
Awali Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema kuwa
tatizo kubwa la vijana hasa wa mkoa wa Arusha wanachokitaka kikubwa sana ni
Pesa na wala sio mawazo mazuri ya upataji
wa pesa na mitaaji imara hivyo bado asilimia kubwa sana ya Vijana
wanabaki wakiwa wanalalamikia Serikali
Mongela alisema kuwa hali hiyo inasababisha vijana kuona
kuwa Serikali haiwathamini,lakini bado Jiji la Arusha limeweka mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawapa fursa vijana wa mkoa wa Arusha sanjari
na kuwaboreshea mazingira mazuri na imara ya kufanyia biashara zao pamoja na
shuguli za kila siku.
MWISHO
No comments:
Post a Comment