NAIBU WAZIRI ASHIKWA NA BUTWAA JUU YA MALIPO YA MKANDARASI UWANJA WA NDEGE KISONGO
NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA
Naibu waziri wa
Uchukuzi mhandisi dkt.Charles Tizeba ameiagiza mamlaka ya Viwanja vya
ndege(TAA) kukaa pamoja na mkarandarasi wa kampuni ya Harising and Sons ili
kukubalina namna ambavyo wanaweza wakafanya marekebisho ya kipande cha barabara
cha mita 420 ili mkandarasi huyo aweze kumaliziwa malipo yake.
Ameyasema hayo
mara baada ya kufanya ukaguzi katika barabara hiyo ya kurushia na kutua ndege
iliyopo ndani katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kisongo nje kidogo mwa
jiji la Arusha.
Dkt.Tizeba
amesema kuwa ni vyema kama pande hizo mbili
zikakaa pamoja ili kupata muafaka kwa kuwa Mhandisi Mshauri alipendekeza
marekebisho yafanyike baada ya msimu wa mvua kumalizika na wamiliki wa viwanja
wanahitaji marekebisho yasisubiri msimu kumalizika.
Aidha amefafanua
kuwa endapo pande hizo mbili zitakubaliana basi ni wazi kuwa mkandarasi
atapatiwa fedha zake zote zilizobakia ambapo amesema kuwa mpaka sasa tayari
ameshapatiwa malipo kwa asilimia 60 tu.
naibu waziri wa
uchukuzi amesema kuwa mradi huo tayari umeshakamilika kilichokuwa kinasubiriwa
ni makabidhiano tu ambapo mkandarasi anaona amefanya kazi vizuri huku mwenye
kiwanja anaona hajakamilishiwa uwanja wao.
Kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege injinia White Majula amesema
kuwa kuotokana na ubovu wa miundombinu uliokuwepo mamlaka ya viwanja vya ndege
imekuwa ikifanya ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha
lami ambapo kwa mwaka 2011-2012 wamekarabati meta 420 kwa kiwango cha lami ili
kukamilisha urefu wa meta 1620 zilizopo.
Pia ametaja
baadhi ya changamoto ambazo bado zinahitaji kupatiwa marekebisho mara moja kuwa
ni pamoja na Mwiingiliano wa barabara ya magari Arusha-Minjingu na miundo mbinu
ya kiwanja ambayo imejengwa ndani ya eneo la kiwanja hivyo kutishia usalama wa
kiwanja ambapo licha ya kujadiliwa na Mkoa wa Arusha,TAA,TANROADS na Wizara ya
Uchukuzi, bado suala la kuhamisha barabara hiyo halijapatiwa ufumbuzi.
Lakini hata
hivyo Injinia Majula amesema kuwa kutokuwepo kwa jengo la Abiria kumeathiri
huduma ya kiwanja kutokana na ufinyu wa bajeti,Mmlaka ya Viwanja vya Ndege
inaendelea kutafuta wabia kupitia sekta binafsi ili kufanikisha mpango huu.
Kiwanja cha
ndege cha Arusha kilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1950,kikiwa kinamilikiwa na
mjasiriamali wa kizungu na kilimilikishwa rasmi serikalini mwishoni mwa miaka
ya 1960 ambapo kina barabara moja ya kuruka na kutua ndege ya kiwango cha lami
yenye urefu wa meta 1620 na upana wa meta 30 inayotumika kwa ndege zenye ukubwa
na uwezo wa kubeba abiria 70 mfano ATR 72.
Mwisho…………………………….
No comments:
Post a Comment