Friday, October 5, 2012

VIJANA WASISITIZWA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI WASIOGOPE MAKADA WA MUDA MREFU WA CHAMA




IMEELEZWA kuwa kutokana na vijana wengi kutokuwa na ujasiri wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kumesababisha baadhi ya viongozi wazee kukaa madarakani kwa muda mrefu huku vijana nao nao wakikosa haki zao za msingi za uongozi kuanzia ngazi ya chama na Taifa kwa Ujumla.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa  wilaya ya Meru Bw Julius Mungure mara baada ya kushinda katika kinyanganyiro hicho ambacho kiliwahusisha makada maarufu wa chama hicho mapema wiki hii wilyani humo

Aidha bw Mungure alisema kuwa vijana wengi sana wanakosa Ujasiri wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuhofia hata umri na ukaada wa baadhi ya viongozi bila kujua kuwa wanapoteza haki zao za  msingi na wanauwezo mkubwa sana wa kuweza kupata madaraka ingawaje wapo baadhi ya watu ambao kila mara wananganagania madaraka

Alifafanua kuwa kwa sasa kuna mabadililiko makubwa sana hivyo vijana nao wanatakiwa kwenda sanjari na mabadiliko hayo na kuhakikisha kuwa wanapiga hatua na kama watafanikiwa kufanya hivyo basi watrachangia sana mabadiliko makubwa ndani ya chama tawala na Jamii kwa ujumla.

“leo mimi nimeweza kuonesha njia ya kuhakikisha kuwa vijana wanaweza kwa kupambana na makada wa muda mrefu sana wa chama hiki na nimeweza kuibuka mshindi tena  kwa kura nyingi sana  sasa nawasihi sana vijana wenzangu tuhakikishe kuwa tunaboresha hata chama chetu kwa kuwa tupo sawa kisheria na kama tutafanya hivi basi tutachangia sana hata kuweza kupunguza vuguvugu la siasa chafu ambazo zinaendelea hapa nchini na ambazo zimekuwa ni chanzo kikubwa sana cha uvunjwaji wa sheria za Nchi’aliongeza Bw Julius

Akiongelea suala zima la kuwasaidia vijana hasa wa wilaya hiyo na mkoa wa Arusha kwa ujumla alisema kuwa anatarajia kupunguza vuguvugu la siasa chafu ambazo zinaendelea hasa kwa wilaya hiyo kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wanatumia fursa mbalimbali ambazo zipo na ambazo zinaweza kuwasaidia kw akiwango kikubwa sana katika kupambana na umaskini.

Alibainisha  kuwa endapo kama vijana hao wataunganika na kukaa sehemu moja basi wataweza kupiga hatua kubwa sana katika maisha na chama kwa ujumla  kwa kuwa kwa sasa bado kuna wimbi kubwa la vijana ambao wanajiingiza katika makundi ambayo hayafai kutokana na uhaba wa elimu hasa ya Ujasiamali ambapo pia hali hiyo ni chanzo kikubwa sana cha siasa chafu kwa kuona kuwa chama tawala hakiwasaidii

‘yapo maneno mengi sana ambayo yanasema huko mitaani kuwa chama tawala hakiwasaidii vijana lakini kwa upande wangu mimi nitahakikisha kuwa hili halipo kwa upande wa wilaya ya Meru halipo kwa kuwa nina uwezo wa kuwapa elimu ya ujasimali na hivyo na kuweza kuwarudisha kwa Chama chetu hasa wale waliopo nje ya kundi letu “aliongeza Bw Julius

Hataivyo katika mnchuano huo Bw Julius alipata kura 575 huku mpinzani wake mkubwa sana ambaye ni kada wa muda mrefu sana wa CCM,Bw Elishilia Kaaya naye alipata kura 213 ambapo pia asilimia kubwa sana ya wapiga kurab katika uchaguzi huo walisema kuwa wameamua kufanya mabadiliko ya hali ya juu sana katika kudumisha Uongozi bora hasa kwa vijana.

MWISHO

2 comments:

  1. KUNA MDAU MMOJA ALITUMA COMMENTS ZAKE KWA NJIA YA SIMU KUWA HATA WALIOKAA MADARAKANI KWA MUDA MREFU WANAWAOGOPESHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA NAFASI ZA UONGOZI KWA HIYO WAZEE WAWACHIE VIJANA NAO WAWEZE KUJINASI

    MTOTO MDAU KUTOKA ARUSHA

    ReplyDelete