RAISI KIKWETE ASISITIZA SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA TAFITI
ZA KILIMO ILI VITAFITI MAZAO MBALIMBALI YA KILIMO
Na Queen Lema,ARUSHA
RAISI Jakaya Kikwete amezitaka Nchi za bara la Afrika
kuhakikisha kuwa zinaboresha vituo mbalimbali vya utafiti wa kilimo kwani kama
kila kituo kitafanya vema tafiti zake basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuimarisha
Kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa zaidi ndani ya nchi mbalimbali ambazo
bado mpaka sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kilimo duni
Raisi Kikwete aliyasema hayo jana(LEO)wakati akifungua
mkutano wa wadau wa mapinduzi ya kijani ya kilimo kwa nchi
mbalimbali za Afrika(AGRA) ambapo alisema kuwa bado sekta ya kilimo katika nchi
mbalimbali inakabiliwa na changamoto kubwa sana hali ambayo inatakiwa
kutatuliwa kwa haraka sana kupitia vituo mbalimbali vya utafiti wa Kilimo
Alifafanua kuwa kwa sasa kunaitajika sana
mapinduzi hasa kwenye taasisi za utafiti kwani hizo ndizo zitakazochochea sana mabadiiliko ya kilimo kutokana na uitaji mkubwa sana ambao upo ndani ya
nchi mbalimbali kwa bara la Afrika
Pia alisema kuwa kama vituo hivyo vya tafiti vitapewa
kipaumbele basi pia vitachangia kwa kiwango kikubwa sana
kuweza kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zinakabili sekta hiyo ya kilimo
pamoja na wakulima ambao wanaitaji msaada mkubwa sana hasa wa wataalamu wa kilimo ambao
wanatokea katika vituo hivyo vya utafiti.
"kwa sasa tuhakikishe kuwa tunajipanga ilivyo kwa kutoa
kipaumbele kwa vituo hivi vya utafiti na hivi vituo navyo vinatakiwa
kuhakikisha kuwa vinajiwekeza zaidi kwa kuwa bunifu na kutafiti hata mazao
zaidi ya mawili kwa mwaka na kama Serikali zetu zitasimamia hivyo basi ni wazi
kuwa zitchangia sana hata ongezeko la chakula na vipato vya wakulima hao kwa
wingi sana"aliongeza Dkt Kikwete
Katika hatua nyingine pia alisema kuwa ili kukuza na
kuimarisha sekta ya Kilimo hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla wadau
mbalimbali wa Kilimo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa mafunzo na elimu zaidi
kwa wakulima hasa wale wa vijijini kwani kutokana na uhaba wa elimu asilimia
kubwa ya wakulima wanafanya kilimo cha mila na desturi huku hali hizo zikiwa
zinachangia kwa kiwango kikubwa sana kudidimiza mazao na kusababisha hata
ukosefu wa chakula.
"kama tutawapa hawa wakulima wetu vipaumbele kwa
kusisitiza zaidi elimu, na maitaji mengine kwa ajili ya kuboresha kilimo basi
wataweza kupiga hatua kubwa sana kutokana na baadhi yao hawana elimu huku jambo
hilo likiwa linachangia sana kilimo duni pamoja na umaskini miongoni mwa jamii
za wakulima"aliongeza Dkt Kikwete
Naye aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa bw Koffi
Annan alisema kuwa ni vema kama wadau wa sekta binafsi na sekta za umma
wakahakikisha kuwa wanawekeza zaidi katika Kilimo ambapo kama watafanikiwa
kufanya hivyo basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana kuimarisha zaidi kilimo
sehemu mbalimbali duniani na hali hiyo itachangia hata uchumi wa Nchi zao
`
Bw Annan alizitaka Serikali za Nchi za Afrika nazo
kuhakikisha kuwa nazo zinakuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa katika kilimo
sanjari na kuwa bunifu katika kuwasaidia wakulima wadogo na wakubwa hasa
kwenye maitaji yao
muhimu ambayo mara nyingine wanayokosa huku hali hiyo ikifanya kilimo kiweze
kudorora na kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment