Sunday, September 30, 2012

TANZANIA KUTENGA BILIONI 30 KWA AJILI YA KUENDELEZA KILIMO



TANZANIA KUTENGA BILIONI 30 KWA AJILI YA KUENDELEZA KILIMO

Na Rose Kitosio,ARUSHA

TANZANIA imetenga kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya
kuendeleza kilimo hasa kuwainua wakulima wa vijijini ambao
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wataalamu na maafisa ugani  wa
kilimo .

Hayo yalisemwa jana na waziri wa kilimo chakula na ushirika Tanzania
Christopher Chiza alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa sekta ya
kilimo  wa mapinduzi ya kijani uliomalizika jana  mjini hapa.

Alisema kuwa tanzani a bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya
kukosekana kwa  wataalamu wa kilimo hali inayopelekea wakulima
wadogowadogo hasa wa vijjiini kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina
tija kwao .

Aidha alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo ya kukosekana kwa
wataalamu wa kilimo wakiwemo  maafisa ugani imekuwa ni sababbu kubwa
ya Tanzania kutofikia katika malengo yake muhimu waliyojiwekea hasa
katika sekta ya kilimo .

“Tanzania bado tunakabiliwa na changamoto ya wataalamu wa kilimo na
hii inasababisha wakulima kuendelea tu na  kilimo ambacho hakina tija
yeyote kwao  hivyo hii bajeti tuliyoitenga tutahakikisha wakulima
wanafikiwa na elimu ambayo itawafanya wapige hatua katika kilimo na
pia kupukana na kilimo cha mazoea”alisema Chiza

Kutokana na hali hiyo waziri chiza alisema kuwa kutokana na bajeti
ambayo Tanzania imetenga watahakikisha kuwa maafisa ugani na wataalamu
watapatikana wa kutosha ili iweze kutolewa  elimu ya kutosha kwa
wakulima ambao wanalima kilimo cha mazoea ili waweze kuondokana na
hali hiyo.

Kwa upandea wake waziri wa maji profesa Jummane  Magembe alisema kuwa
kwa sasa kuna uharibifu wa vyanzo vya majiunaotokana na kuchoma misitu
kwa ajili a kilimo ,mila potofu ,uwindaji,kufyeaka maeneo ya vyanzo
,kuchoma mkaa  hivyo kusababisha kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi
ambayo yamekuwa yakiathiri kilimo  cha Tanzania.

Magembe aliongeza kuwa ni vema watanzania wakajikita zaidia katika
kutumia nishati ambazo hazichangii kuleta uharibifu wa mazingira kama
vile nishati ya umeme wa jua ambapo endapo wananchi watatumia nishati
hizo ni wazi kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi hayatakuwepo tena

No comments:

Post a Comment