NA MERY KITOSIO, MERU
SHIRIKA la
Afrika Amini Alama kutoka nchini Austria
limewakutanisha wanafuzi zaidi ya elfu moja kutoka shule mbali mbali za msingi na sekondari wilayani arumeru kwa lengo la kutambua na kukuza vipaji
vyao walivyo navyo ili waweze kusaidiwa kielimu .
Akizungumza
na upako wa habari meneja wa shirika hilo bw Willium Kinua alisema kuwa shirika hilo
limeamua kuwakutanisha wanafunzi hao kwa kuwa wapo wanafunzi wenye vipaji
lakini havitumiki ipasavyo.
Alisema kuwa
kupitia tamasha hilo la kutambua wanafunzi wenye vipaji litasaidia kwa kiwango kikubwa kuibua vipaji
mbali mbali ambavyo wameshindwa kuviibua ambapo kupitia michoro ambayo
watachora itawasaidia kupatiwa misaada mbali mbali ya kielimu.
Aliongeza
kuwa shirika hilo kwa sasa limelenga
kuwasaidia watoto kwa kuangalia vile vipaji muhimu walivyozaliwa navyo ikiwa ni
wale wenye vipaji vya sanaa,uchoraji pamoja na mpira ambapo
wanafuzi wengi wanashindwa kujitambua ni vipiji gani walivyo navyo.
“Afrika
Amini Alama tumejipanga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliopo haya maeneo
wananufaika na elimu kwa kupitia vipaji vyao walivyo navyo kwa kuwa tumeona
wako wanafunzi wengi wana vipaji vyao vya kuzaliwa lakini hawajitambui ni
kipaji gani walicho nacho”alisema Kinua.
Kwa upande
wake mratibu wa shirika hilo bw Jaffarson Severua alisema kuwa awali kabla ya kufanyika
kwa tamasha hilo la kukuza vipaji shirika hilo liliwapatia kwanza wanafuzni hao
semina kwa ajili ya kujua namna ya kuibua vipaji vyao ambapo mara bada ya
kuibua vipaji hivyo kwa njia ya uchoraji picha hizo zitapelekwa Austria ambapo
wafadhili wa shirika hilo ndio watawajibika kuwasaidia wanafunzi hao .
Aidha
Severua alitaja maeneo waliyotokea wanafunzi hao kuwa ni kata za
Ngarenanyuki,Ngabobo,Kisimiri,Olkwang’ado,Momela,Lendoiya,pamoja na Miririn
zote zikiwa za halmashauri ya Meru.
Hata hivyo
aliiomba serikali kuwaunga mkono hasa pale wanapokwama hasa kielimu kwa kuwa
wamejikita zaidi kusaidia zile jamii zisizokuwa na uwezo wa kuendeleza watoto
kielimu ambapo hadi sasa wana mkakati wa kujenga shule nne za awali ambapo hadi
sasa wameshajenga katika kata ya leguruki na ngarenanyuki shule zenye
majaengo yanayogahrimu zaidi ya shilingi
milioni 300.
mwisho
No comments:
Post a Comment