Na Queen Lema,MERU
SHIRIKA LA AFRIKA AMINI LAWAKUTANISHA
WANAFUNZI ELFU MOJA ILI KUKUZA VIPAJI
SHIRIKA la Afrika Amini Alama kutoka nchini Austria
limewakutanisha wanafuzi zaidi ya elfu moja kutoka shule mbali mbali za
msingi na sekondari wilayani arumeru kwa lengo la kutambua na
kukuza vipaji vyao walivyo navyo ili waweze kusaidiwa kielimu .
Akizungumza na Majira meneja wa shirika hilo bw Willium Kinua alisema kuwa shirika hilo limeamua
kuwakutanisha wanafunzi hao kwa kuwa wapo wanafunzi wenye vipaji lakini havitumiki
ipasavyo.
Alisema kuwa kupitia tamasha hilo la kutambua wanafunzi wenye vipaji
litasaidia kwa kiwango kikubwa kuibua vipaji mbali mbali ambavyo
wameshindwa kuviibua ambapo kupitia michoro ambayo watachora itawasaidia
kupatiwa misaada mbali mbali ya kielimu.
Aliongeza kuwa shirika hilo kwa sasa
limelenga kuwasaidia watoto kwa kuangalia vile vipaji muhimu walivyozaliwa
navyo ikiwa ni wale wenye vipaji vya sanaa,uchoraji pamoja na mpira
ambapo wanafuzi wengi wanashindwa kujitambua ni vipiji gani walivyo
navyo.
“Afrika Amini Alama tumejipanga kuhakikisha kuwa
wanafunzi wote waliopo haya maeneo wananufaika na elimu kwa kupitia vipaji vyao
walivyo navyo kwa kuwa tumeona wako wanafunzi wengi wana vipaji vyao vya
kuzaliwa lakini hawajitambui ni kipaji gani walicho nacho”alisema Kinua.
Kwa upande wake mratibu wa shirika hilo bw
Jaffarson Severua alisema kuwa awali kabla ya kufanyika kwa tamasha hilo la
kukuza vipaji shirika hilo liliwapatia kwanza wanafuzi hao semina kwa ajili ya
kujua namna ya kuibua vipaji vyao ambapo mara bada ya kuibua vipaji hivyo kwa
njia ya uchoraji picha hizo zitapelekwa Austria ambapo wafadhili wa shirika
hilo ndio watawajibika kuwasaidia wanafunzi hao
Aidha Severua alitaja maeneo waliyotokea
wanafunzi hao kuwa ni kata za
Ngarenanyuki,Ngabobo,Kisimiri,Olkwang’ado,Momela,Lendoiya,pamoja na Miririn
zote zikiwa za halmashauri ya Meru.
Hata hivyo aliiomba serikali kuwaunga mkono hasa
pale wanapokwama hasa kielimu kwa kuwa wamejikita zaidi kusaidia zile jamii
zisizokuwa na uwezo wa kuendeleza watoto kielimu ambapo hadi sasa wana mkakati
wa kujenga shule nne za awali ambapo hadi sasa wameshajenga katika kata ya
leguruki na ngarenanyuki shule zenye majaengo yanayogahrimu zaidi ya
shilingi milioni 300.
mwisho
No comments:
Post a Comment