Na Queen Lema, MERU
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari,
ameishauri Serikali hasa kwa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaweka mikakati
zaidi hasa kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na uelewa
mdogo, pamoja na kushindwa kusoma na kuandika kupewa muda wa ziada na fursa
nyingi zaidi za muda wa masomo ili kuweza kupunguza idadi hiyo ambayo
itapunguza changamoto hiyo ambayo inaikabili shule nyingi sasa.
Alisema kuwa kwa sasa wanafunzi ambao hawajui kusoma na
kuandika pamoja na wale wenye uelewa mdogo huwa wanaachwa kama
walivyo huku muda wa masomo nao ukiwa unaendelea hali ambayo ndiyo inayochangia
hata maendeleo hafifu ya Elimu kwa baadhi ya wilaya hapa nchini
Bw Nassari aliyasema hayo wakati wa maafali tisa ya darasa la saba katika shule ya
Fikiria Kwanza Usa river wilayani Meru Mkoani hapa mapema jana ambapo
pia alisema kuwa ipo haja ya Serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika masuala
ya Elimu hasa kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto kama hiyo mkoani
hapa.
“tusilie kila siku elimu elimu bali tunapaswa kuangalia changamot ambazo
zinaikabili sekta hiyo tena hasa katika wasiojua kusoma na kundika pamoja na
wale wenye uelewa finyu lakini kama wanafunzi hawa tutakuwa tunawaacha kama
hasara ya mzazi basi tutakuwa tunaongeza idadi ya Mambumbu ila kama
tutaweka Nia hata kwa kuwapa walimu kazi
ya ziada ya kuwafundisha hawa watoto basi kiwango cha elimu kitakuwa kwa kiwango
kikubwa sana’aliongeza
Alisema kuwa mbali na changamoto ambazo zinaonekana kuwa
chanzo cha kusababisha elimu hasa ya Mkoa wa Arusha kuwa chini pia Serikali
inatakiwa kuhakikisha kuwa inaangalia zaidi shule za Kata kwani nazo zimekuwa
shule ambazo zinasahaulika sana na kusababisha hata aina ya elimu ambayo
inatolewa ndani ya shule hizo kuwa ni elimu duni sana huku asilimia kubwa ya
watanzania wakiwa wanategemea elimu kutoka ndani ya shule hizo
“kwa upande wa Vijijini shule hizi ni tegemeo kubwa sana kwa
jamii lakini sasa hapa inaonekana baadhi ya watendaji wa Serikali kukwepa majukumu yao na kusababisha mfumo wa elimu
hizi kuwa chini lakini kama wangekuwa wanazitatua kero mbalimbali basi hata
idadi ya watoto wenye uelewa finyu na wale wasiojua kusoma na kuandika nayo
ingepungua sana na hivyo kukuza hata kiwango cha elimu ya Meru na Mkoa wa
Arusha kwa Ujumla”aliongeza Bw Nassari
Hataivyo Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo ya Fikiria kwanza
Bi Necta Lema alisema kuwa ili kuboreesha suala zima la elimu hapa nchini kwa
ujumla nazo shule mbalimbali zinatakiwa kutatua kero za elimu ambazo zipo
sanjari na kuhakikisha kuwa wanajiwekea taratibu za kuwapa Motisha walimu mara
kwa mara ili kuongeza hata kiwango cha ufaulu kwa haraka sana
Bi Lema alibainisha kuwa kwa sasa zipo baadhi ya shule ambazo
zinawasahau sana walimu katika kuwapa Motisha hali ambayo inawafanya walimu wa
shule hizo kuweza kufundisha kwa njia ya mazoea tofauti na pale ambapo walimu
watakapotangaziwa Motisha kuweza kufundisha
kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuwa mfano mzuri kwa shule na hata mbele
ya wanafunzi.
“Motisha kwa walimu ni jambo jema sana
kwani sisi tayari mpaka hapa tumeshajaribu kuweza kufanya hivyo na matunda
tumeyaona hivyo ni jukumu la kila mkuu wa shule kuhakikisha kuwa mbalina
kukazania elimu bora lakini kuwa mbunifu na ubunifu huo utachangia sana kuweza kuongeza hata
idadi ya wanafunzi ambao wanafranya vema zaidi “aliongeza Bi Lema
No comments:
Post a Comment