Na Ashura Mohamed,Arusha
JAJI
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jaji Aisha Nyerere,amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kuweza kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni juu ya
katiba mpya.
Aidha mashirika,taasisi zilizo za kiserikali au
zisizokuwa za kiserikali kutumia nafasi zao kuisaidia serikali kuhamasisha umma
juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.
Jaji Nyerere aliyasema hayo juzi mjini hapa
wakati alipokuwa akizindua vitabu vya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii pamoja
na kitabu kinachohusu haki za jamii katika maeneo ya uwekezaji,uzinduzi ulioenda
sambamba na maadhimisho ya miak 17 ya Kituo cha sheria na haki za
binadamu(LHRC).
“Napenda niwakumbushe watanzania kuwa kwa sasa
taifa letu lipo katika mchakato wa kutunga katiba mpya,mchakato huu upo katika
hatua za mwanzo kabisa ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi,hivyo kwa kuzingatia
hayo napenda kuwahimiza ninyi na raia wengine kushiriki kikamilifu kikamilifu
kutoa maoni yenu”
“Kituo cha sheria na haki za binadamu pamoja na
watu wengine wenye nafasi na uwezo wa kutoa elimu kwa uumaa kushiriki kikamilifu
katika mchakato mzima,mnapaswa kutumia vema nafasi zenu”alisema na kuongeza
Jaji huyo alisema kuwa watetezi wa haki za
binadamu wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali hivyo wanapaswa kuungwa
mkoni kwani utetezi wa haki za binadamu ni wajibu wa jamii nzima.
“Watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuisaidia
serikali katika uendelezaji na kulinda haki za binadamu na ni nafasi pekee
kutengeneza misingi imara ya kuwatetea na kuwalinda watetezi wa haki za
binadamau na kuna nafasi nzuri kama wakati huu wa mchakato wa kuhakikisha kuwa
haki za binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanaridhiwa na kuwekwa
katika katiba mpya kwani hii itakuwa na mchango mkubwa sana katika kulinda haki
za binadamu na watetetzi wa haki hizo”alisema Jaji Nyerere
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo
hicho Dk.Hellen Kijobisimbo alisema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa
ziliwakabili katika kutekeleza majukumu yao ni pamoja na sheria kwua
kandamizi,hata wanapokuwa wanapokuwa wanamsaidia mtu kisheria,sheria zimekuwa
zikiwakandamiza.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la
mfumo wa mahakama ambapo mashauri yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi
kukamilika,wasaidizi wa kisheria kutokutambulika.
Dk.Hellen aliongeza kuwa vyombo vya dola navyo
vimekuwa ni tatizo kwao kwani wakati mwingine wao wakiwa katika majukumu yao ya
utetezi,vyombo vya dola vimekuwa vikiwaona wao ni wapinzani wakati wao ni
wasaidizi wa serikali.
Naye Mratibu wa Kitengo cha uwajibikaji wa
makampuni na mazingira(LHRC) Wakili Flaviana Charles akizungumza wakati wa
uzinduzi wa vitabu hivyo alisema kuwa sheria ya uwekezaji hapa
nchini haina vifungu vyenye kutoa wajibu wa wawekezaji kwa wananchi jambo
linalosababisha jamii kutokunufaika na miradi ya uwekezaji inavyotekelezwa
katika maeneo husika.
Aliongeza kuwa ukosefu wa sheria inayosimamia
uwajibikaji wa makampuni kwa jamii umepekelea kuwepo kw augumu wa kuzichukulia
hatua za kisheria kampuni zinazoshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii,ambayo
imesababisha uwepo kwa migogoro isiyoisha ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment