Na Mustafa Leu. ARUSHA
TUME ya taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini Tacaids, imeshauriwa kuongeza
kasi zaidi ya mapambano hayo dhidi ya maambukizi mapya kwa kutoa
elimu zaidi kwa jamii iweze kuchukua hatua za kujiepusha na
maambukizi na kusathiri nguvu kazi ya taifa inayotegemewa.
Hayo
yameelezwa jana na Afisa tawala mkoa wa Arusha, Exaud Mwanga,alipokuwa
akifungua kikao cha siku moja cha viongozi wa madhehebu ya dini mkoani
Arusha kuhusu mwitikio na usahiriki wao katika mapambano ya ugonjwa wa
ukimwi kilichoaandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiyi ukimwi nchini
Tacaids.
Mwanga, amesema kuwa serikali inatambua juhudi kubwa
zinazofanywa na madhehebu ya dini kwa kushirikiana na tacaids na
wadau wengine kwa kutoa ushauri wa kiroho kwa watu
waishio na ukimwi ushauri unaowawezesha waliokwisha ambukizwa kuishi
kwa matumaini ..
Amesema mchango unaotolewa na madhehebu ya dini
katika kupunguza ongezeko la maambukizi ya ukimwi ni mkubwa sana
,pamoja na mchango huo kuwa mkubwa bado mahitaji ya elimu ni makubwa
hasa ngazi za kata, vijiji na jamii na familia yanahitajika ili
kupunguza ongezeko la maambukizi mapya ambapo kwa mijini kiwango cha
maambukizi ni asilimia 8.7 na vijini ni asilimia 4.7
Awali
Kamishina wa tume ya ukinmwi nchini Askofu mstaafu wa KKKt, Peter
Lukumbusho Mwamasika , amesema taasisi za dini zina wajibu mkubwa
kutoa misaada ya kimalezi, kiafya, kielimu, kiushauri, kisheria kwa
waathirika ambao ni waumini wao ili waepuke kupata maambukizi mapya.
Amesema
taasisi hizo za dini lazima zitambue kuwa zina wajibu wa kuwatunza
yatima na wajane wasiokuwa na uwezo ambao wanatokana na
vifo vya ukimwi ili kuwaanzishia miradi ya kiuchumi na kuachana na
tabia ya kuwaombea dua na kuwaacha waende zao bila kuwawezesha
Amewaambia
viongozi hao kuwa Tacaids ina jukumu kubwa la kuhamasisha watu waeleze
mahitaji yao kuhusu mapambano dhidi ya ukimwi na kuwaepushia kupata
maambukizi mapya na kupitia Tacaids, serikali inzifikia taasisi za dini
ili ziweze kusaidia kutoa elimkwa wananchi kuhusu madhara ya ukimwi na
hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi mapya.
mwisho
No comments:
Post a Comment