NA MERY KITOSIO, MERU
VIONGOZI mbali mbali wa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi
ya kata ,vijiji na vitongoji wametakiwa
kushughulika na kero za wananchi na kuhakikisha kuwa wanazitatua kwa muda
muafaka ili wananchi wao waone umuhimu wa chama na serikali .
Hayo yalisemwa na
katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya arumeru bw Langaeli akyoo alipokuwa
akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa chama cha
mapinduzi uliofanyika kijiji cha ngyeku kata ya kikatiti wilayani a rumeru.
Alisema kuwa kwa sasa ufike muda viongozi wasionekane kuwa
wamepewa uongozi kwa ajili ya kustarehe na badala yake wajikite zaidi katika
kusikiliza matatizo ya wananchi wao kwa kuwa uongozi wao ndio kimbilio la
wananchi kwa kuhakikishwa wanawasikiliza
yale wanyohitaji.
Alieleza kuwa ili wananchi waweze kukiamini chama cha mapinduzi ni vema viongozi hao wakadili
na matatizo mbali mbali yaliyoko ndani ya jamii husika hususan kuwatatulia kero
ya maji kwa kuwa viongozi hao wao ndio
suluhisho la wananchi .
Alifafanua
kuwa kwa sasa hakuna tena haja ya kutafuta wa chawi wanaosababisha ccm
kuchukiwa bali viongozi watambue kuwa
wenyewe ndio wasababishaji kwa kuwa
hawafuatilii ipasavyo kutatua kero zinazowakabili wananchi wao
“Ninawaagiza madiwani , wenyeviti wa
vijiji na vitongoji kuhakikisha mnafuatilia kero hizo ,tusitafute wachawi
wanaosababisha CCM, kuchukiwa wakati wachawi ni nyie wenyewe”alisema Akyoo.
Mbali na hayo akyoo akielezea
mafanikio ya serikali ya ccm katika kijiji hicho cha ngyeku alisema kuwa ni
pamoja na kufanikiwa kujenga shule ya sekondari ngeku,zahanati pamoja na
barabara iliyotengenezwa kwa mradi wa tasaf.
Aidha katika mkutano huo wananchi wa
eneo hilo walitoa kilio chao cha maji wanachokabiliwa nacho kwa katibu huyo ambapo alitumia fursa hiyo
kumuagiza mara moja diwani wa kata hiyo kuhakikisha kuwa anatatua tatizo hilo
kwa haraka iwezekanvyo.
Hata hivyo katika mkutano huo jumla
ya wanachama 24 walijiunga na chama
hicho ambapo watatu walitoka chama cha demokrasia na maendeleo huku wengine 21
wakiwa wananchama wapya.
No comments:
Post a Comment