WAMILIKI, WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA MFANO MZURI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Na Queen Lema, ARUSHA
WAMILIKI na Wakuu wa shule mbalimbali kwa kanda ya kaskazini
wameombwa kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa kuhakikisha kuwa wanawapa fursa
wanafunzi mbalimbali kuwa mabalozi na
waelimisha rika kuhusiana na Mazingira ili kuendelea kuhifadhi mazingira ambayo yanaharibiwa kila mara
kuanzia ngazi ya shule.
Mratibu wa shirika la Roots and Shoots la mkoa wa Arusha Bw
Japhet Mwanangombe alitoa wito huo wakati wa maafali ya pili kwa waelimishaji
rika 191 ambao wameitimu kwa kupata elimu ya sekondari pamoja na elimu ya
uelimishaji rika mapema jana.
Alisema kuwa kwa sasa pamoja na kuwa wamejikita kuhakikisha
kuwa kila shule inakuwa na vitalu kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi umuhimu
wa kuhifadhi mazingira lakini bado kuna baadhi ya walimu wamekuwa kikwazo
kikubwa kwa kutowapa wanafunzi fursa mbalimbalin za kupambana na uharibifu wa
mazingira.
Kufuatia hali hiyo alisema kuwa inachangia sana
wanafunzi kukosa haki yao ya msingi hali ambayo
inachangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya
wanafunzi hao kuwa maadui wa mazingira badala ya kuwa marafiki wa mazingira kwa
maslahi ya maisha yao
ya baadaye na jamii ambazo zinawazunguka
“tunachoomba ni kuwa baadhi ya wamiliki wa shule pamoja na
wakuuu wa shule ambao bado wanaona suala la kuwa na elimu ya mazingira si
rafiki sana kwao kwa kweli wanakosea kwani wanasababisha sana hawa wanafunzi
wawe na maadui wa mazingira kwa kuharibu hata vyanzo mbalimnbali lakini
kutokana na hali hiyo kama shule itashirikiana na taasisi mbalimbali kama
yetu basi watachangia sana ufanisi
katika suala la mazingira”alisema
Pia alisema,nazo shule ambazo zipo pembezoni mwa miji nazo
hazipaswi kukaa bila ya kuwa na elimu ya mazingira hasa katika mchakato mzima
wa Upandaji wa vitalu ndani ya shule zao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatafuta
elimu hiyo kwa haraka sana kwani hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya mazingira
ambayo inaanzia kuanzia ngazi ya Shule inasababisha sana mazingira ya Vijijni kuendelea kuharibiwa.
Katika hatua nyingine alisema kuwa Shirika hilo limejipanga kuhakikisha kuwa linaendelea
kuzalisha waelimisha Rika wengi zaidi hasa kwenye suala zima la Mazingira kwani
mpaka sasa zaidi ya waelimisha Rika 235 wa
wilaya 22 za Kanda ya Kaskazini
wameshanufaika na elimu hiyo ambapo hata hali ya uharibifu wa mazingira nayo
imepungua ndani ya shule mbalimbali tofauti na hapo awali
“leo hawa Vijana wameitimu ambao pia ni wahitimu wa darasa
la saba na kidato cha nne lakini pia wanaelimu hii sasa sisin tunachokifanya ni
kuhakikisha kuwa tunawatuma ndani ya wilaya zetu 22 ili wakapunguze huko tatizo
la uharibifu wa mazingira ambao unafanywa na baadhi ya wanajamii kutokana na
uhaba wa elimu”aliongeza Bw Joseph
Kwa upande wa wahitimu wa uelimishaji rika ambao wameitimu
kwa kupata elimu hiyo kwa zaidi ya miaka minne walisema kuwa pamoja na kuwa
wamefanikiwa kupata elimu hiyo kwa uraisi sana lakini navyo vijiji hasa vya nje
ya Miji vinatakiwa kuhakikisha kuwa wanawatumia ili kupunguza athari mbalimbali
ambazo zinajitokeza mara kwa malra ndani ya jamii.
MWISHO
No comments:
Post a Comment