WANAWAKE WA KIMERU WAMTAHADHARISHA MBUNGE WAO
DHIDI YA KAULI ZAKE
Na Queen Lema,ARUSHA
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wanawake wa
eneo la kisambare Usariver Wilyani Meru mkoani Arusha wamesema kuwa kamwe
hawatavumilia kauli za mbunge wa jimbo hilo bw Joshua Nasari badala yake
watalazimika kuingia barabarani hata kwa vita na kumpinga hadharani
Mbunge huyo kwani kauli zake hazijengi hoja za kutetea shida za wananchi
na badala yake kauli zake zinachochea Malumbano pamoja na Migogoro huku
wanawake wa Vijijini wakiwa wanakabiliwa na shida mbalimbali
Wanawake hao waliyasema hayo jana wilyani humo
wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao waliwatembelea Kijijini humo
sanjari na kuongea na wanachama wa chama cha mapinduzi
Wanawake hao walisema kuwa kauli za Mbunge
Nassari sio kauli za kujenga bali ni kauli za kubomoa na kuchochea malumbano
makubwa sana
ambapo pia kwa sasa mbunge huyo angepswa kuongelea changamoto mbalimbali ambazo
zimo kwenye jamiii
Walifafanua kuwa mbunge huyo anapaswa kujua na
kutambua kuwa alipewa jimbo hilo kwa hasira kutokana na kukithiri kwa
changamoto lukuki ambazo zimo kwenye jamii hasa za Wameru na kwa hali hiyo huu
ndio muda muafaka wa mbunge huyo kuhakikisha kuwa anatatua kero na wala sio
kutoa matammko ambayo hayana tija na jamii
Waliongeza kuwa kauli hizo lzimekuwa na madhara
makubwa sana hasa kwa vija na kwa kuwa mpaka sasa wapo baadhi yao wanaofanya
makosa kwa visingizo vya Mbunge huyo hali ambayo ni chanzo kikubwa sana cha
uharibifu wa Amani
“tunachotaka kujua ni kuwa tunatatuliwa kero
zetu lakini badala mbunge afikirie suala zima la maendeleo yeye anafikiria
kuzima mwenge wakati sisi hatuna shida na mwenge na mwenge unapita lakini shida
zetu hasa sisi wakina mama wa Nkoakirika hatujui hata majira ya saa sasa
tueleweje kwani tukimbia CCM kutokan a na changamoto lakini hii ya sasa ni kali
na kama huyu mbunge ataendelea hivi basi ipo siku matatizo makubwa sana
yatatokea”waliongeza wakina mama hao huku wakiwa wanalia
Mbali na hayo waliongeza kuwa nao viongozi wa
siasa watakiwa kkukumbuka ahadi mbalimbali ambazo wamezitoa kwa jamii hasa
nyakati za kampeni kwani baadhi ya viongozi hasa wa Mkoa wa Arusha wakishapata
nafasi ya kuongoza basi wanakuwa na matamko ambayo hayana tija kwa jamii na
badala yake matamko hayo yanasabahbisha hata baadhi ya vijana kushikwa shikwa
ovyo na Polisi
Awali Katibu wa CCM Wilaya ya Meru bw Langaeli
Akyoo alikiri kuwa chama cha mapinduzi kilikuwa na kasoro hali ambayo
iliwafanya wananchama wake kukopesha jimbo la Arumeru Mashariki lakini kwa sasa
chama hicho kimejipanga hata kwa Watendaji wa huduma zote za kijamii
kuhakikisha kuwa wanatekeleza Sera za wananchi
Bw Akyoo alifafanua kuwa hasira ambazo
ndio chanzo pekee cha wananchi kutoa kura kwa upinzani kwa sasa
zitapunguzwa kwa kiwango cha juu huku jamii hasa za vijijini zenye
maitaji maalumu nazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao kwani
uwezekano wa kuwasaidia bado ni mkubwa sana.
No comments:
Post a Comment