CHANZO CHA HABARI Na Queen Lema, ARUSHA
Imeelezwa kuwa idadi ya wanawake wajawazito waliohudhuria
vituo vya afya kwa mwaka 2011 na kupima virusi vya ukimwi walikuwa
48375 ambapo kati yao 1677 walikuwa
wameathirika na Ukimwi huku wilaya za longido na Karatu zikiwa zinaongoza kuwa
na idadi kubwa sana kwa mwaka 2011 mkoani Arusha.
Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa
Arusha(Mount Meru) Dkt Omary Chande wakati akiongea
katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari mapema jana mkoani hapa.
Aidha Dkt Chande
alisema kuwa walifanikiwa kujua
na kutambua kuwa idadi hiyo ya wanawake imeathirika mara baada ya kufanya
vipimo maalumu ambavyo vinafanywa kabla ya kufikia hatua ya uzazi ili kuepusha
madhara ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“leo tunaweza kusema ,kuwa ndani ya wanawake hawa ambao
wamefanikiwa kupimwa Ukimwi ambao ni kama asilimia 3 wameonekana kuathirika
lakini ili kuokoa maisha ya mama na mtoto tulichokifanya ni kuhakikisha kuwa
tunawapa elimu ya kujikinga na kuwalea watoto wao vema”aliongeza Dkt Chande.
Awali alisema kuwa zipo wilaya ambazo zinaongoza katika
maambukizi ya Mama wajawazito ambapo Wilaya za Longido, na Karatu, na Manispaa
ya Arusha zilionekana kukithiri kwa waathirika kutokana na kuwepo kwa migongano
ya kijamii ambayo ndiyo chanzo kikubwa sana
cha Magonjwa hayo
“hapa ukiangalia ndani ya Wilaya ya longido kuna maambukizi
ya Ukimwi kwa kiwango cha asilimia 14, ikifuatiliwa na Karatu, kwa asilimia
4.7, huku nyingine ikiwa ni Manispaa kwa asilimia ni asilimia 4 hali ambayo kwa kweli ni tishio
kubwa sana lakini tunajikita sana kuhakikisha kuwa hawa watoto wanaozaliwa
wanakuwa katika hali ya usalama zaidi”aliongeza Dkt Chande
Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa mwaka 2011 pia watoto
zaidi ya 928 walikutwa wakiwa na virusi vya ukimwi ambapo kati yao asilimia 82
walinyosnyeshwa maziwa ya mama zao ambapo asilimia 18 walikuwa wanatumia njia
mbadala ili kuendelea kuishi.
Pia alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 takwimu
zinaonesha kuwa waki mama ambao wamejifungua hospitalini ni 33,643 ambapo kati
ya hao 1907 hawakuwai kufika katika vituo vya afya wakati wakiwa wajawazito na
hivyo hii kupelekea kuwepo kwa asilimia 6 ya wanawake ambao hawaeleweki kuwa kama wana maambukizi au hawana
Dkt huyo aliongeza kuwa kati ya hao asilimia 4 walikutrwa
wakiwa tayari na maambukiz ya Ukimwi mara baada ya kupimwa huku wakiwa na
ujauzito hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa changamoto hasa kwenye idara
ya uzazi salama.
Hataivyo alitaja changamoto kubwa sana
ambayo inaikabili idara lhiyo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa amasa ndogo sana ya wanaume ambao wamekuwa wakijitokeza kupima virusi vya
ukimwi wakifuatana na wake zao katika vituo mbalimbali vya Afya,
Alifafanunua kuwa changamoto hiyo imekuwa ikichangiwa na
mambo mbalimbali ndani ya jamii za kitanzania ikiwemo ukosefu wa elimu kwa
makundi hayo, mila na desturi zilizopo katika jamii mbalimbali,pamoja na hali ya uchumi hivyo juhudi za lazima
zinahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali katika kutoa elimu hiyo ili kuondokana
na changamoto hizo
Mwisho
No comments:
Post a Comment