VYAMA VYA SIASA ARUSHA VYATAKIWA KUTOA ELIMU YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA VIJANA ILI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MALI
Na Queen Lema, ARUSHA
VYAMA vya siasa hasa kwa mkoa wa Arusha vimeombwa kuhakikisha kuwa vinatoa elimu ya
Uraia pamoja na umuhimu wa demokrasia
kwenye siasa kwani kutokana na hilo
asilimia kubwa ya Vijana wanaharibu sheria hizo bila kujua na kutambua kuwa
wanafanya kosa
Hayo yameelezwa na Bi Cristanta Mwinyi ambaye ni Katibu wa CCM Kata ya Ngararenaro
wakati akiongea na vyombo vya habari mara
baada ya kuvamiwa na vijana wa
Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)na kuharibu mali zenye thamani
ya zaidi ya Laki tano
Bi Mwinyi alisema kuwa pamoja na kuwa wamevamiwa na vijana
hao wenye itikadi tofauti hapo juzi bado kuna nafasi kubwa sana ya kuweza kuhakikisha kuwa vijana hao
wanajua na kutambua maana halisi ya Demokrasia
Aliongeza kuwa vijana hao ambao si mara ya kwanza kufanya
matukio kama hayo wanafanya hivyo kwa kujua kuwa wanashabikia baadhi ya vyama
na kuharibu mali
ya chama kingine wanavunja hata sheria na taratibu za nchi na pia ni chanzo
hata cha mauji ambayo hayana tija kwa
jamii
Alifafanua kuwa endapo vyama vya siasa vingekuwa na tabia ya
kuwaonya vijana wake kuacha kuharibu au kufanya fujo kwa vyama pinzani basi
siasa ya mkoa wa Arusha ingekuwa inaenda vema tofauti na sasa ambapo siasa
imegeuka kama uwanja wa mapambano makali
kutokana na itikadi kali
“hawa vijana wanapotoka katika mikutano yao si mara mara ya
kwanza kuharibu ofisi hii sasa kama wataendelea hivi kuharibu mali za ofisi hii
ni wazi kuwa ipo siku na vijana wetu nao watainuka na hawatakubali na hayo
yatakuwa ni mauji ya hali ya juu sasa ni wakati wa Vyama vya siasa kuhakikisha
kuwa wanaliangalia suala hili kwa undani sana ili kuepusha madhara kama hayo”aliongeza
Bi Mwinyi
Alifafanua kuwa endapo kama Siasa itaenda kistaarabu hasa
pale ambapo baadhi ya vijana hao watakuwa wamepata elimu ya Uraia na Demokrasia
basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata
kuweza kuwapa wananchi wengine fursa ya
kutumia Demokrasia vema tofauti na pale wenye itikadi moja kwenda nyingine kwani
uharibifu huo nao unachangia sana
hata Umaskini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment