MAJAMBAZI YAKAMATWA NA POLISI JIJINI ARUSHA
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha
Bw.Liberatus Sabas akiwa anawaonyesha waandishi wa habari risasi,pisto
na kifaa cha kunyooshea risasi jana ofisini kwake.
Wanachi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu mara baada ya kugongwa na gari jana katika barabara ya katimakutano jijini Arusha
NA MAHMOUD AHMAD -ARUSHA
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata
majambazi sugu watatu kwa nyakatitofauti wakiwa na silaha aina ya pisto
yenye risasi tano pamoja na mashine ya kunyooshea bunduki , kifaa cha
kubustia risasi pamoja na risasi 46 za bunduki aina ya smg Katika
matukio mawili tofauti.
Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa
polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa matukio hayo mawili
yalitokea kwa nyakati tofauti Katika maeneo tofauti ya mkoani hapa
kufuatia msako mkali uliokuwa ukifanya na jeshi la polisi kwa
kushirikiana na wananchi wasamaria wema.
Kamanda alisema kuwa Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni
jambazi sugu aliyejihusisha na matukoi ya hivi karibuni aliyefahamika
kwa jina la Salimu Kiwele alimaarufu kwa jina la Msaula(39)mkazi wa
sombetini mkoani hapa akiwa na mke wake aliyetambulika kwa jina la
Princes Juma (34) wote ni wakazi wa sombetini wamekamatwa nyumbani
kwao wakiwa na silaha pamoja na risasi.
Alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa na silaha aina ya
pisto Glock FFN 350 ikiwa na risasi tano ambazo zilikuwa ndani ya
magazine ya silaha hiyo.
Alisema kuwa mtu huyu pamoja na mke wake walikuwa
wanatafutwa na polisi kwa kipindi cha mda mrefu kufuatia kuhusika na
matukio mbalimbali ya uhalifu ,mauaji pamoja na wizi ambao ulishawahi
kutokea jijini hapa .
Hata hivyo Sabas alisema kuwa Katika tukio lingine
mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Konsolata Tarimo (30)mkazi
wa ngaramtoni amekamatwa na jeshi la polisi akiwa na risasi 46 za
bunduki aina ya smg pamoja na vifaa mbalimbali za bunduki hiyo ikiwemo
kifaa cha kusafishia silaha hiyo.
Alibainisha kuwa mwanamke huyo alikutwa nyumbani kwake
majira ya saa nane usiku kuamkia September 6 wakati askari waliokuwa
doria walipofanya msako wa kushutukiza Katika nyumba hiyo baada ya
kutilia shaka.
Alisema kuwa askari hao walipofanya msako huo walikuta
risasi hizo 46 za bunduki hiyo aina ya smg ,muhuri ambao ulikuwa
umeandikwa pande zote mbili huku pande ya kwanza ikiwa imeandikwa
District game office simanjiro na upande mungine umeandikwa district
game of monduli district,kifaa cha kubusti risasi Katika bunduki hiyo ya
smg pamoja na kifaa cha kusafishia silaha hiyo inayotumiwa na risasi
hizo.
Aidha alibainisha kuwa silaha ambayo ilikuwa inatumika kwa
ajili ya silaha hiyo haijakamatwa bali msako mkali unaendelea ili
kukamata silaha hiyo iliyokuwa ikitumia risasi hizo.
Alisema kuwa watuhumiwa wote bado wapo chini ya ulinzi
kwa ajili yamahojiano na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa
mahakamani haraka iwezekanavyo.
Wakati huo huo Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Ibrahimu
Saloni(30) mkazi wa sakina amefariki dunia mara baada ya kugongwa na
gari aina hince na kupoteza maisha papo hapo
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi
Mkoani hapa alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi jioni
katika barabara ya makao mapya mtaa wa levolosi jijiji hapa .
Alisema kuwa mtu dereva wa gari hilo aina ya hince yenye namba za usajili T225 BZE alitambulika kwa jina la Shaban Mohamed (27)mkazi wa tengeru. Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea barabara kuu kuelekea barabara ya kati makutano ndipo dereva hoyo alimgonga mwendesha baskeli
Shuhuda wa Ajali hiyo Bi.Ashura Ali ambaye shughuli zake ni
mamantilie alisema kuwa hiyo ni mara ya pili kwa ajali kutoke katika
eneo hilo na huku wanaogogwa kupoteza maisha kutokana na mwendo kasi wa
maderevaAlisema kuwa mtu dereva wa gari hilo aina ya hince yenye namba za usajili T225 BZE alitambulika kwa jina la Shaban Mohamed (27)mkazi wa tengeru. Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea barabara kuu kuelekea barabara ya kati makutano ndipo dereva hoyo alimgonga mwendesha baskeli
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
Wananchi wenye hasira kali wamemtupia lawama mkandarasi
anayeshughulikia barabara zote za katikati ya Mji wa Arusha hususani
brabara ya kati makutano mtaa wa Levolosi kwa kutoweka matuta wala alama
za barabarani yanayodhibi mwendo kasi hali inayopelekea ajali za mara
kwa mara kutokea huku Viongozi husika wakifumbia macho
No comments:
Post a Comment