WATU ZAIDI YA 500 WAMEFARIKI DUNIANI MKOANI ARUSHA KUTOKANA NA AJALI
Na Queen Lema, ARUSHA
IMEELEZWA kuwa kutokana na changamoto mbali mbali za uasalama barabarani kwa mkoa wa arusha zimesababisha zaidi ya watu 441 kupoteza maisha kutokana na ajali za magari huku watu zaidi 120 nao wakipoteza maisha kwa ajili ya ajali za pikipiki kwa kipindi cha januari 2010 hadi agost 2012.
Hayo yalielezwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kwa mkoa wa arusha bw Mwakyoma Marison wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbali mbali wa usalama barabarani katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama kwa mkoa wa arusha mapema jana.
Alisema kuwa ajali hizo zimetokana na vyanzo mbali mbali ambavyo vinafahamika na jamii ya mkoa wa arusha ambapo ni pamoja na uzembe wa madereva, uzembe wa watembea kwa miguu,ubovu wa magari, ubovu wa barabara pamoja na chanzo kikubwa cha ajali ambazo ni mwendo kasi
Alibainisha kuwa hali hizo zimekuwa ni changio kubwa sana la ajali za barabarani ingawaje kikosi cha usalama wa barabara kimejipanga kihakikisha kuwa kuanzia sasa ajali hizo zinapungua kwa kiwango kikubwa sana kwa kuwachukulia hatua kali na za kiesheria wale wote ambao wanasababisha ajali hizo za mara kwa mara.
Awali aliongeza kuwa pamoja na kuwa na mikakati imara ambayo itasababisha Ulemavu wa ajali pamoja na vifo kupungua kwa kiwango kikubwa sana lakini bado kuna changamoto kubwa sana hasa upande wa Manispaa ya Arusha ambapo napo changamoto hizo zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana lili kupunguza hata tatizo hilo
Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha bw John Mongela alisema kuwa ajali inafanya nguvu kazi ya Taifa kupungua sana na hivyo ni jukumu la kila mtu kuanzia ngazi ya familia kuhakikisha kuwa anawapa hata watoto elimu hiyo ili kupunguza hata kasi ya Ajali
MWISHO
No comments:
Post a Comment