NA BERTHA ISMAIL, ARUSHA
Watoto
wenye walemavu waishio mkoani Arusha waililia serikali juu ya kuboresha
mfumo wa elimu hasa sekondari unaowatenga hali inayowafanya kukata
tamaa ya kuthamini elimu.
Akiongea na gazeti hili kilipotembelea
shule ya msingi Meru kwa niaba ya wanafunzi wenzake wenye ulemavu wa
aina tofauti tofauti Brenda honest mwenye ulemavu wa kutosikia
alisema kuwa mfumo wa elimu hasa wa shule za sekondari haiwajali wala
kuthamini walemavu kama wao.
Brenda aliendelea kusema kuwa ingawa
wao ni walemavu lakini jamii itambue kuwa ulemavu huo hawakuuchagua
hivyo ameiomba serikali na jamii yote kwa ujumla kuwasaidia kwa
kuwasapoti katika mambo mbali mbali zitakazowawezesha kujitegemea hapo
baadae na siyo kuwa tegemezi siku zote za maisha yao.
Akitolea
mfano mambo wanayohitaji kuungwa mkono Brenda alisema kuwa mfumo wa
elimu hasa katika shule za sekondari
na kuendelea, haijawapa kipaumbele walemavu hasa wa kusikia, kuona,
wenye mtindio wa ubongo n.k kwa uboresheji vifaa vya kufundishiwa,
walimu maalum kwa ajili yao pamoja na punguzo la ada hali itakayowafanya
kupata moyo wa kusoma.
"kutokana na hayo basi, sisi walemavu
tunalia na serikali kwa kuendelea kututengenezea mazingira ya sisi
tuendelee kuwa watu tegemezi badala ya kujitegemea wenyewe kiuchumi hapo
baadaye kwani kuna wenzetu wengi tu wamefundishwa vizuri shuleni hapa
walipoenda secondari wakashindwa masomo na kukata tamaa baada ya kuona
hawaelewi masomo lakini wanaendelea kusogeza madarasa" alisema Brenda
"Mbali
na kuililia serikali kupewa upendeleo wa kielimu, pia sisi walemavu
wasichana mashindano mengi ya kitaifa tumekuwa tukishuhudia kwa wenzetu
tu lakini sisi hatushirikishwi hali inayotufanya kujiona tumetengwa
zaidi hivyo nitumie nafasi hii kuiomba serikali itambue mchango wa
walemavu kiuchumi, kijamii, na hata kisiasa pindi
tunapopiga kura kuwaweke madarakani"alimalizia Brenda.
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo ya msingi Meru, ambaye pia ni
mlezi mkuu wa watoto walemavu wawapo shuleni Bwana Mussa Luwambano
alisema kuwa katika shule Meru wana watoto 76 wenye ulemavu tafauti
tofauti ambapo hafundishwa zaidi ya miaka saba ikilinganishwa na wenzao
wasio walemavu.
Akielezea changamoto kubwa wanayokumbana nazo
katika kuwawezesha wenye ulemavu kupata elimu itakayowasaidia katika
maisha yao hapo baadae katika kujitegemea Luwambano alisema kuwa ni
ukosefu wa vifaa vya kufundishia pamoja na usafiri maalum hali
ambayowalemavu wamekuwa wakichelewa shule sambamba na baadhi yao
kupoteza maisha kwa kugongwa na magari hasa viziwi wasiosikia milio wala
honi za magari.
Pia aliongeza kuwa mbali na hilo pia mfumo wa
elimu ya walemavu haujajizatiti katika elimu ya sekondari kwa kuwepo na
walimu maalum wa kuwafundusha, madarasa, vifaa na hata miundo mbinu kwa
ujumla hali inayosababisha baadhi ya watoto kuishia elimu ya msingi na
kuendelea kuwa tegemezi kwa zinowazunguka kitendo ambacho ni kikwazo
kikubwa kwa uchumi wa nchi yetu.
"Baada ya kuona watoto wengi
tunaowafundisha wakifaulu kwenda sekondari hurudi kwa kushindwa masomo,
tumeamua kuwajengea chuo cha ufundi ili wamalizapo elimu ya msingi
angalau wajiendeleze kiufundi, hivyo serikali hasa halmashauri yetu ya
jiji la Arusha , taasisi ,mashirika na watu binafsi wajitokeze kuisaidia
chuo hicho kukamilika ili watoto hawa wajiendeleze kiufundi kuliko
kubaki mitaani na kuwa ombaomba"Alisema mwalimu Luwambano.
Aidha
pia mwalimu Luwambano aliwataka wananchi kutambua kuwa malezi ya watoto
ni jukumu kila mmoja wetu bila kujali ni mlemavu au laa hivyo wajitokeze
kuwasaidia pindi wawaonapo wamepata shida hasa wakiwa barabarani
wawavushe kuepusha kugongwa na
magari.
............. MWISHO
No comments:
Post a Comment