Friday, September 28, 2012

mkutano wa mapinduzi ya kijani wajadili hatma ya wakulima wadogo barani afrika






ALIYEOKO KUSHOTO NI BI BELINDA BILLGATE WAKATI WA KATI NI RAISI JAKAYA KIKWETE, NA WA KULIA NI BW KOFF ANNAN KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAPINDUZI YA KIJANI KWA NCHI ZA AFRIKA MAPEMA JANA, PICHA NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA






Na Queen Lema, ARUSHA

KOFFI ANNAN AWATAKA VIONGOZI WA NCHI ZA BARA LA AFRIKA KUHAKIKISHA KUWA WANAPA FURSA MBALIMBALI WAKULIMA WA VIJIJINI ILI KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WATU MIJINI

ALIYEKUWA katibu mkuu wa umoja wa Mataifa bw Koffi Annan amewataka viongozi mbalimbali katika nchi za bara la afrika kuhakikisha kuwa wanawajengea wakulima hasa wa vijijini uwezo wa kulima kwa kujiamini ili kuweza kupunguza wimbi kubwa la watu wanaokimbilia zaidi mijini

bw Annan aliyesema hayo leo (Jana) wakati alipokuwa akiongea na vyombo katika mkutano wa mapinduzi ya kijani unaondelea mjini hapa

Aidha bw Annan alifafanua kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa vijijini wanakimbilia zaidi mijini kutokana na kukosa misaada ya kilimo huku hali hiyo nayo ikichangia kwa kiwango kikubwa sana ongezeko la watu

Aliongeza kuwa endapo kama viongozi hao watafanikiwa kuwaboreshea wakulima hata maslahi ya kilimo basi watachangia sana hata kuondokana na tatizo la machafuko mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea ndani ya nchi mbalimbali za bara la Afrika kutokana na uhaba wa cahakula

'kama hawa viongozi wa bara la Afrika wakidhamiria sana hasa kwa wakulima wale wa vijijini kuhakikisha kuwa wanawapa fursa mbalimbali ambazo sehemu nyingine hamna basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuweza kuweka uhakika wa chakula ndani na nje ya nchi zao lakini kama watakuwa hawawapi fursa basi watachangia sana hata kuweza kuwadidimiza wakulima hao wa chini'aliongeza bw Annan

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa sasa ni muda wa bara la Afrika kuhakikisha kuwa mafanikio kuelekea kufikia malengo ya millenia yanaendelea kuwa ya kuhamsisha zaidi mageuzi ya kilimo ili kuweza kuimarisha hata uchumi wa kijamii kwani kilimo hasa kwa bara la Afrika lina uwezo huo

Mbali na hayo alisema kuwa kwa muda huu ni vema kama kukawa na ushirika bunifu miongoni mwa sekta za Umma na zile binafsi ambapo kupitia sekta hizo zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kutoa njia ambazo zinaweza kusaidia kufikia mafanikio ya kilimo hasa vijijini.

Awali Waziri wa kilimo chakula na ushirika hapa nchini bw christopher chizza alisema kuwa kwa sasa nchi ya Tanzania ina mikakai mingi sana ya kuhakikisha kuwa inaboresha kilimo chake kwa kutoa fursa mbalimbali za Kilimo ambacho kina uwezo wa kubadilisha hata Uchumi wa nchi

Bw chizza alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania kwa sasa imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wakulima wengi wa sasa wanatumia zaidi kilimo cha Umwagiliaji ambacho ni kilimo cha kudumu tofauti na kilimo cha kutegemea zaidi msimu wa mvua ambao mara nyingine unabadilika badilika na kusababisha hasara kwa wakulima na watumiaji wa mazao mbalimbali

"kwa sasa tumehakikisha kuwa tumejiwekeza zaidi katika aina ya kilimo cha umwagiliaji ambacho ndicho ,kinachoweza kubadilisha hali za wakulima wetu na sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha wakulima wote wanakubali hili ili kuweza kuinua hata aina ya kilimo chetu'aliongeza bw Chizza.

MWISHO


No comments:

Post a Comment