Sunday, October 7, 2012

ZAIDI YA WANANCHI 6000 KUPEWA ELIMU YA MAZINGIRA NA SHERIA ZAKE




Na Queen Lema,ARUSHA

ZAIDI ya wakazi 6000 kutoka katika kata ya daraja mbili mkoani hapa wanatarajiwa kufikiwa na elimu ya mazingira ingawaje kwa sasa bado mitaa mbalmbali ya Kata hiyo inaongoza kwa uchafu na  uharibifu wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vyanzo vya maji hali ambayo inachangia mlipuko wa magonjwa na ukame

Hayo yameelezwa jana na mtatibu wa shirika la Initiative for youth(INFOY) bw Laurent Sabuni wakati akiongea na wananchi wa mitaa mbalimbali ya Kata hiyo ambayo bado inakabiliwa na tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira kutokana na uhaba wa elimu ya utunzaji wa mazingira

Bw Laurent alisema kuwa wananchi hao watafanikiwa kupatiwa elimu kuanzia sasa ambapo elimu hiyo italenga kufanya kata hiyo kuwa katika hali ya usafi kwani kwa sasa hali ya usafi katika kata hiyo ni mbaya sana hususani kwa nyakati kama hizi ambazo Mvua zinatarajiwa kuanza kwa wakati wowote ule.

Alisema kuwa wamelazimika kutoa elimu hiyo ili kufanya kata hiyo na mitaa yake kuwa na usafi wa kutosha ilin kuepusha madhara mbalimbali ambayo yanajitokeza kutokana na uchafu uliokithiri pembezoni mwa barabara na hata katika vyanzo mbalimbali vya maji hususani Mito ambayo inazunguka kata hiyo

“tumelezimika kushirikiana na wenzetu wa Foundation for Civil Society kuweza kuokoa afya za watu hawa 6000 ambao miongoni mwao wapo watoto kwani hali ya usafi  bado ni ndogo sana ingawaje kwa sasa Jiji linahimiza kufanya hivyo sasa kwa hiyo hawa watakaopata elimu hii tunatarajia kabisa wataweza kufanya mabadiliko makubwa sana”aliongeza Bw Laurent

Pia alisema kuwa ili kuhakikisha zoezi hilo la kuokoa maisha ya watu wa kata hiyo ya daraja mbili linafanikiwa kwa kiwango kikubwa pia wamefanikiwa kujiwekea taratibu mbalimbali ambazo zitatumika kulinda mazingira mbalimbali ya Kata hiyo ambapo taratibu hizo zitawafanya wachafuzi wa mazingira kuepukana na tabia hiyo kwa kuhofia kufikishwa mahakamani na kutozwa faini kubwa sana

Alibainisha kuwa nazo kata nyingine zinatakiwa kuhakikisha kuwa zinakuwa na sheria kali sana hasa kwa wachafuzi wa mazingira kwani bado jamii inakabiliwa na watu hao  kwa kuwa wanafikiri kuwa sheria hazipo na kama zipo hazitekelezwi huku hali ikisababisha baadhi ya mitaa ya Jiji la Arusha kukithiri kwa kiwango kikubwa sana cha uchafu

“Mitaa kupitia Serikali zake zinatakiwa kuhakikisha kuwa sheria mbalimbali za utunzaji wa mazingira zinafutwa lakini kama sheria zitakuwa zinawekwa maofisini pekee na kushindwa kufafanuiliwa kwa wananchi huku hali ikisababisha baadhi ya watu kutumia fursa hiyo kuchafua mazingira ovyo na kufanya hata jitiada mbalimbali za wadau wa mazingira kushindwa kutekelezwa kwa wakati”alisema Bw Laurent

MWISHO

No comments:

Post a Comment