Friday, October 19, 2012

NHC YATAKIWA KUFUATA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA



NHC YATAKIWA KUFUATA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba (NHC), Nehemia Kyando Mchechu.
…………………………………………
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
 KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) imeliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA) katika utendaji wake wa kazi.
 Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa POAC,Kabwe Zitto wakati kamati hiyo ilipokutana na baadhi ya viongozi  kuhusu kuzungumzia utendaji wa shirika hilo kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya Bunge  jijini Dares Salaam.
   Maagizo hayo yalitolewa na kamati hiyo kufuatia shirika hilo katika  mwaka wa fedha 2010/2011  lilipanga kutumia sh.bilioni 31 lakini limetumia  sh. bilioni sh. bilioni 25  nje ya taratibu za PPRA.
 Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Nehemia Msechu alisema  suala hilo limetokana nakuwepo kwa miradi ya dharura  iliyoangalia masuala ya kibiashara. Hata hivyo  alisema  eneo hilo ni moja ya changamoto wanayokabiliana nayo, hivyo wameshaanza kuifanyia kazi kushirikiana na PPRA.
 Kamati hiyo pia imelitaka shirika hilo, kuwakilisha matumizi ya fedha ya mwaka huu unaoishia Juni, 2012 kwa kuonesha mchanganuo sahihi kabla kikao kijacho na kubadilisha mfumo wa utaratibu wa malipo ya fedha taslimu,badala yake watumie benki ili kulinda mapato ya shirika.
 Aidha Mwenyekiti wa kamati hiyo alilipongeza shirika hilo kwa  kwa kujiendesha kifaida kutoka sh. bilioni tatu hadi kufikia sh.bilioni sita na thamani ya mali za shirika hilo kwa sasa  imefikia sh. trilioni 1.75.
 Zitto aliongeza kuwa shirika hilo linatakiwa kuendelea mchakato wa  kujiendesha kama kampuni ili liweze kupata mtaji wa kutosha.
Kamati hiyo ilitaka shirika hilo, kuzingatia mpango wa kujenga nyumba zenye gharama nafuu kwa watu wenye kipato cha chini hususan maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment