Tuesday, October 23, 2012

SERIKALI YATAKIWA KUTOA RUZUKU KWA SHULE ZA PEMBEZONI


SEIKALI imetakiwa kuzipa ruzuku kubwa shule za pembezoni ili kuwezesha shule hizo kupata vitendea kazi vya masomo na miundo mbinu bora  yatakayoweka   mazingira sawa ya ushindani kitaaluma katika mitihani ya kitaifa.

Shule nyingi za pembezoni zinadaiwa kukosa mabweni ,madarasa ,maabara na waalimu wa kutosha hali inayowanyima wanafunzi walio wengi wanaosoma katika shule hizo kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa.

Akihutubia wananchi katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Soit Sambu Wilayani Ngorongoro mratibu wa shirika la misaada la Focus On Tanzanian Communities Happy Mwamasika alisema mazingira ya shule za vijijijini ni mabaya na magumu.

“Ni wazi sote leo tunajionea mazingira ya shule hii ,haina hata maabara ya somo la sayansi  na watoto wanafundishwa  masomo hayo hapa watawezaje kufanya mitihani ya masomo hayo na kufaulu kama wengine wa mijini”alihoji Mwamasika.
Alisema kuwa ni lazima kuwepo kwa mazingira ya haki ili kuondoa matabaka na ubaguzi katoka mfumo wa Taifa wa elimu.

Alisema kuwa shirika hilo litajenga bweni la kisasa litalaoweza kuchukua wanafunzi zaidi ya mia moja na kupunguza msongamno katika bweni moja lililopo ambalo wanafunzi watatu wanalala katika kitanda kimoja.

“Nimetishwa na mazingira niliyoyaona bweni lillopo linapaswa kuchukau wanafunzi themanini lakini wanalala watoto zaidi ya mia mbili hali hii inatisha”alisema Mwamasika.

Aliwataka wananchi wa eneo hilo na wazazi wa wanafunzi kuchangia maendeleo ya shule hiyo na kuwato wasiwasi kwa kuiwa wajumbe wote wa bodi ya wakurugenzi ya FOTZC wanatambua  umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike na kwamba hilo  litajengwa hivi karibuni.

Aidha alitambua mchango wa kampuni ya kitalii ya  Thomson kwa kulipa shirika hilo fursa ya kutangaza ashughuli na kupata michango kutoka kwa wahisani mbalimbali wa miradi ya kijamii.

“Naishukuru kampuni hii kipekee  wasingetupa fursa ya kutangaza kazi zetu kupitia makambi yao, leo hii tusingeweza kuwa na nyumba za walimu katika shule hii wala tusingekuwa katika mchakato wa kujenga bweni la wasichana tutakalolijenga mwishoni mwa mwaka huu”alisema Mwamasika.

Alisema kuwa kampuni ya Thomson ni mfano tu wa namna ya  kuonyesha ni  kwa jinsi gani jamii zinaweza kunufaika na utalii endapo utafanywa kwa dhamira ya kuendeleza jamii na bila upotoshwaji.

No comments:

Post a Comment